POLISI YAZIMA MAANDAMANO YA WAUMINI WA KKKT...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/polisi-yazima-maandamano-ya-waumini-wa.html
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Jimbo la Arusha Magharibi wanaliotarajiwa kuandamana kushinikiza kurejeshwa kazini kwa Mchungaji Philemon Mollel leo hawatafanya hivyo.
Hatua hiyo ilifikiwa jana na Jeshi la Polisi la Mkoa, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya Jeshi hilo, kwamba waumini hao wameshauriwa kuwataka wazee 50 wa Usharika wa Ngateu kuorodhesha majina na saini zao na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa.
Chanzo chetu cha habari ndani ya Jeshi hilo, kilisema lengo ni kutaka kuwasilisha malalamiko yao kwa Mkuu huyo kwa njia ya maandishi na kisha kukaa pamoja kutafuta mwafaka badala ya kuandamana.
Habari zilisema kuwa sababu ya Polisi kuzuia maandamano hayo inatokana na wiki jana Jeshi hilo kuzuia maandamano ya Waumini wa kiislamu wa Msikiti wa Ijumaa yaliyokuwa na lengo la kuelezea matatizo katika Msikiti huo.
“Kama Polisi ingeruhusu maandamano haya ya KKKT huku ikiwa imezuia ya Waislamu, ni dhahiri ingeonekana inapendelea na hivyo kusababisha tafsiri mbaya kwa umma … tunadhani hatua hii ya kujiorodhesha ni nzuri,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa.
Maandamano hayo ambayo awali yalitarajiwa kufanyika Jumapili ijayo, yalikuwa yamepangwa kuanzia Kiranyi katika Jimbo la Arusha Magharibi la Kanisa hilo hadi makao makuu ya Dayosisi hiyo kumshinikiza Msaidizi wa Askofu Mkuu, Solomon Massangwa amrudishe Mchungaji Mollel kazini.
Maandamano hayo yangeanza saa 4 asubuhi na pia yangemshinikiza Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Israel ole Karyongi kujiuzulu kwa tuhuma za kuisababishia Dayosisi hasara ya mabilioni ya fedha na kufikia hatua mali za Kanisa hilo kutaka kupigwa mnada.
Mchungaji Mollel ambaye alikuwa Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Ngateu, alifukuzwa kazi kutokana na kile viongozi wake wanachodai kuwa ni kufanya makosa yasiyovumilika.
Hata hivyo, kufukuzwa kazi kwa Mchungaji huyo kulitokana na msimamo wake wa kupinga ufujaji wa mali za Kanisa hilo unaodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo wa Dayosisi hiyo hadi kufilisi mali za Kanisa.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, maandamano hayo yalipangwa kuongozwa na vijana wa kimasai, morani, ambao wangevalia lubega na kushirikisha pia waumini wa sharika zingine za jimbo hilo la Arusha Magharibi.
Katika maandamano hayo, taarifa zilisema waumini na morani hao walipanga kubeba biblia, misalaba na mabango yenye ujumbe kuhusu hali ya sintofahamu inayoendelea ndani ya Kanisa.
Mchungaji Mollel alifukuzwa kazi na kuzuiwa kufanya shughuli za kichungaji katika usharika wa Ngateu katika jimbo hilo tangu Desemba 24 mwaka jana kwa kilichoelezwa kuwa ni kufanya vitendo visivyovumilika ndani ya Kanisa.
Kwa mujibu wa waumini wa Usharika wa Ngateu, uongozi wa Usharika uliandika barua kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD) Januari 8 ya kutoa taarifa juu ya maandamano hayo ya amani.
Kiongozi wa kwaya ya usharika huo ambaye pia ni mwanakamati wa maandalizi ya maandamano hayo, Peter Mbise alisema maandamano hayo yangepitia barabara ya Nairobi hadi Sanawari na kuingia barabara ya Afrika Mashariki.
Mbise alisema maandamano hayo pia yangepitia barabara ya Boma na kuingia barabara ya India ziliko ofisi za Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Alisema baada ya kutoa ujumbe kwa Msaidizi wa Askofu, maandamano hayo pia yangekwenda makao makuu ya KKKT nchini na kutoa ujumbe maalumu kwa Mkuu wa Kanisa hilo nchini, Askofu Dk Alex Malasusa.
‘’Tayari tumeshawajulisha wenzetu Polisi kuwa tutakuwa na maandamano hayo ya amani kesho (leo) ambayo yataanzia hapa kanisani Kiranyi na kuelekea ofisi ya Msaidizi wa Askofu na baada ya hapo tutakwenda makao makuu ya Kanisa letu,’’ alisema
‘’Kila muumini atakuwa na Biblia, Msalaba na majani na wengine tutabeba mabango yenye ujumbe tofauti kwa viongozi wetu wa Kanisa juu ya ufisadi wa mali za Kanisa na kutaka wamrudishe Mchungaji Mollel kuendelea na kazi bila masharti yoyote,’’ alisema.
Waumini hao wamekuwa wakihamasishana kwa kutumiana ujumbe mfupi katika simu za mkononi ili kuhakikisha maandamano hayo yanapata watu wa kutosha.
“Bwana Yesu asifiwe mpendwa. Tunaomba Ijumaa saa 4 asubuhi kutakuwa na maandamano kuanzia kanisani Kiranyi kuelekea Dayosisi juu ya ufisadi, hoteli imeuziwa matajiri 17 na ni mali ya washarika.
“Toa taarifa kwa watu zaidi ya 20. Mbiu tunamtaka mchungaji wetu Philemon,” ilisema sehemu ya ujumbe huo uliotumwa kwa waumini jana.
Wakati hayo yakijiri, viongozi wa juu wa Dayosisi hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara watatu wamepanga mbinu za kushughulikia viongozi sita wa Usharika wa Ngateu wakiwamo wachungaji watatu wa Arusha Magharibi.
Vyanzo vya habari kutoka ofisi za Dayosisi vilisema mkakati huo umepangwa na matajiri hao kwa kilichoelezwa kuwa ni kukerwa na taarifa za mara kwa mara zinazotolewa na viongozi na wachungaji hao (majina tunayo) juu ya ufisadi ndani ya Kanisa hilo.
‘’Unajua hawa matajiri wanataka fedha zao milioni 100 walizonunulia hisa kwa siri hawakutaka zijulikane, sasa ndio maana wanapanga mkakati huo mchafu, lakini sijui kama watafanikiwa,’’ alisema mtoa habari ambaye aliogopa kutajwa jina kwa kuogopa kushughulikiwa.
Mwandishi alishuhudia matajiri hao wakiwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa kutwa nzima jana wakimsubiri Kamanda wa Polisi wa Mkoa aliyekuwa katika mkutano ili watimize matakwa yao.