KOCHA PEP GUARDIOLA SASA ATUA RASMI BAYERN MUNICH...

Timu ya soka ya Bayern Munich ya Ujerumani muda mfupi uliopita imefanikiwa kumnasa aliyekuwa kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kwa kumsainisha mkataba wa miaka mitatu kukinoa kikosi hicho kinachoongoza ligi kuu ya nchi hiyo 'Bundesliga' msimu wa 2013/14.
Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni siku chache baada ya kocha huyo kutangaza nia yake ya kurejea tena dimbani akionesha wazi hamu yake ya kufanya kazi katika Ligi Kuu ya Uingereza. Haikuwa hivyo na sasa ametua Ujerumani.
Guardiola alijizolea umaarufu akiwa na kikosi cha Barcelona kutokana na kuweza kutwaa mataji lukuki akiwa na kikosi hicho ambacho kimekuwa hakishikiki kabla ya kupokwa ubingwa wa Hispania na Real Madrid. Baada ya hapo kocha huyo aliamua kupumzika.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item