SISTA ADAIWA KUFUMANIWA NA MUME WA MTU SUMBAWANGA...

Aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki  Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani  ambaye kwa sasa anaishi  nje ya nyumba ya  utawa  eneo  la Kantalamba  mjini hapa, amepandishwa kizimbani akidaiwa kufumaniwa na mume wa mtu.
Katika shauri hilo katika Mahakama ya  Mwanzo mjini hapa mbele ya Hakimu Meddy Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa.
Hata  hivyo, mtawa huyo alionekana kutotulia sehemu moja katika  eneo hilo la Mahakama na alitoweka ghafla kesi ilipotajwa mahakamani hapo.
Katika hati ya madai inadaiwa kuwa mshitakiwa alifumaniwa  na Asteria akiwa na mumewe ambaye jina halijafahamika wakiwa chumbani kwenye nyumba ya kulala wageni ya Chipu iliyoko eneo la Katandala mjini Sumbawanga.
Hakimu Mkinga alipotaja kesi hiyo, mdaiwa hakutokea kwenye  chumba  cha  Mahakama  ikamlazimu aiahirishe hadi Januari 21 na mshitakiwa yuko nje kwa kuwa shauri hilo la madai halina masharti ya dhamana.
Baadhi  ya watawa wa kike  ambao hawakuwa tayari majina yao yaandikwe walikiri  kumfahamu  mlalamikiwa  kwamba alikuwa mtawa wa Shirika  la Masista  wa Maria Mtakatifu Malkia  wa Afrika (MMMA) ambapo  wanadai aliachana na maisha ya utawa kwa hiyari yake miaka miwili  iliyopita.
“Sisi tutamwombea mwenzetu huyo kwa sala … tuliishi naye lakini aliamua tena bila shuruti  kuachana na maisha  haya  ya  utawa … aliaga  na kuomba apumzike  kwa miezi kadhaa uraiani ili ajifikirie kurejea au kuachana na maisha haya.
“Sisi kama watu wazima, tulimwelewa anamaanisha nini sasa ndiyo haya yamemkuta, tutaendelea kumwombea katika  sala  zetu za kila siku,“ alisema mmoja wao.
Yasinta  ambaye  ni  mhudumu  wa afya  katika  hospitali ya mkoa  wa Rukwa mjini hapa amekuwa gumzo karibu kila  kona mjini hapa kutokana na shauri linalomkabili mahakamani.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item