MTOTO AMUUA MWENZAKE KWA KUMCHOMA KISU SHINGONI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/mtoto-amuua-mwenzake-kwa-kumchoma-kisu.html
Kamanda David Misime. |
Akisimulia kisa hicho cha kusikitisha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), David Misime alisema kifo hicho kilitokea Januari 5, mwaka huu saa mbili asubuhi katika kitongoji cha Magungu, Kijiji cha Mpendo wilayani Chemba wanakoishi.
Kamanda Misime alisema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa Tony na Somei walikuwa wanacheza nje nyumbani kwa akina Somei.
Wakati wakicheza, Somei alirusha kisu kwa lengo la kumuua ndege aliyekuwa juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yao.
Hata hivyo kisu hicho kiligonga kwenye mti huo na wakati kinadondoka kilimjeruhi Tony kwa kumchoma shingoni na kusababisha kifo chake.
Kamanda Misime alisema sheria haiwezi kuchukuliwa dhidi ya Somei kwa kuwa ni mtoto na hawezi kuwajibika kwa vitendo vyake.