MUUAJI WAHALIFU ACHAGUA ADHABU YA KUFA KWA UMEME...

KUSHOTO: Robert Gleason akisindikizwa na polisi mahakamani mwaka 2010. PICHA NDOGO: Gleason anavyoonekana sasa. KULIA: Kiti cha umeme alichochagua Gleason kuondoa uhai wake.
Robert Gleason Jr. alitarajiwa kuingia katika chemba ya mauti mjini Virginia usiku wa jana na kufungwa kwenye kiti cha umeme kinachotumika kwa nadra mno, na kuashiria mwisho wa harakati za maombi yake kuharakisha kifo.
Gleason anasema sio kwamba anataka kufa, lakini afadhali sababu anafahamu ataua tena endapo hatamalizwa. Tayari alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kwa kumuua mfungwa mwenzake na kisha kuapa kuendelea kuua isipokuwa akihukumiwa kifo.
Pale mfumo uliposhindwa kuharakisha vya kutosha, akamnyonga mwenzake mwingine na kuonya kwamba idadi ya miili itaendelea kuongezeka kama hawatafanyia kazi tahadhari zake. Gleason alisamehe mapingamizi yake, na kubaki katika mapambano ya kisheria na wanasheria wake wa zamani walioweka pingamizi kujaribu kuokoa maisha yake dhidi ya  matakwa yake.
Kwa nini inarefushwa? Matokeo ya mwisho yanaweka kuwa kama hayo," Gleason alisema kutoka kwenye kusubiria kifo katika sauti nzito ya lafudhi ya Boston kwenye moja ya mahojiano mengi aliyofanya na The Associated Press katika kipindi cha miaka mitatu. "Sehemu ya kifo hainisumbui. Hii nilikuwa naisubiria kwa kitambo kirefu sana. Inaitwa karma."
Gleason alikuwa amepagwa kufa majira ya Saa 3 usiku wa jana katika kituo cha kurekebisha tabia cha Greensville kilichoko Jarratt. Watuhumiwa wenzake wa Virginia aliofungwa nao jela wanaweza kuchagua kati ya kufungwa sindano ya sumu au kuuawa kwa umeme, na Gleason ni mfungwa wa kwanza kuchagua kufa kwa umeme tangu mwaka 2010.
Chaguo hilo lisilo la kawaida linafuatia mfululizo wa matukio mengine ya kushitusha.
"Inatakiwa kuzuiwa. Njia pekee ya kusitisha ni kuniweka katika orodha ya kifo," aliieleza AP wakati huo, akirejea vitisho vyake mahakamani katika matukio kadhaa.
Wakati akisubiria hukumu katika gereza lenye ulinzi wa hali ya juu kwenye milima ambalo linahifadhi wafungwa hatari zaidi nchini, Gleason alimnyonga Aaron Cooper mwenye miaka 26 kwa kupitia waya wa uzio unaotenganisha vizimba vyao kwenye uwanja wa burudani.
Gleason anadai aliwaua wengine - pengine dazeni zaidi - lakini amekataa kutoa maelezo zaidi. Anadai kuwa yeye ni tofauti na wanaume wengine katika orodha ya kifo ya Virginia kwa sababu moja tu muhimu: yeye anaua tu wahalifu.
Watson alikuwa akitumia kifungo cha maisha kwa kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili. Cooper alikuwa mporaji magari akishirikiana na genge la wahuni.
"Sisemi mimi ni mtu bore kwa kuua wahalifu, lakini sikuwahi kuua watu wasio na hatia," alisema Gleason. "Nimeua watu walioishi maisha kama yangu, na wanajua, hivi vitu vinaweza kutokea."
Gleason anasema ni yeye aliyetaka kifo ili kutimiza ahadi kwa wapendwa wake kwamba hataua tena. Alisema kufanya hivyo kutamwezesha kuwafunza watoto, wakiwamo watoto wake wawili wa kiume, kinachoweza kuwapata kama watafuata nyayo zake.
"Sikuwa pale kama baba na ninatumaini kwamba ninaweza kufanya kitu kimoja kizuri cha mwisho," alisema. "Natumaini hiki ni kitu kizuri."
Gleason mwenye miaka 42, alizaliwa huko Lowell, Mass., kijana anayejisikia ambaye bado anasaini barua zake kama 'Bobby kutoka Boston.' Baada ya kumaliza shule ya sanaa huko North Carolina, Gleason alipata tuzo ya msanii wa tattoo kwenye maduka kote katika East Coast. Alitulia kwa muda mrefu nje ya Richmond, akimiliki duka la michoro ya tattoo na kushikilia dini. Kisha baadaye alisema alivutiwa na alijifanya kuvutiwa na dini ili kunufaisha biashara yake ya tattoo.
Wanaoafiki adhabu ya kifo wanasema kwamba kumwacha hai Gleason kunaweka wengine kwenye matatizo. Wapinzani wa adhabu ya kifo wanasema kwamba uhakika kwamba anauawa ulimpa jeuri ya kuwaua Watson na Cooper.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item