UWANJA WA NDEGE JULIUS NYERERE WAKITHIRI KWA WIZI WA MADINI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/uwanja-wa-ndege-julius-nyerere.html
Sehemu ya mbele ya Uwanja wa Ndege wa JNIA, Dar es Salaam kama inavyoonekana wakati wa usiku. |
Biashara haramu na utoroshaji madini nchini hufanywa kwa kiasi kikubwa kwenye viwanja vya ndege nchini hasa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa kutumia ndege zinazosafiri usiku.
Kadhalika, baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni wanaonunua madini nchini, wamekuwa wakitapeliwa madini hayo kwenye uwanja wa JNIA na baadhi ya wafanyabiashara maarufu Dar es Salaam ambao huchukua malipo ya awali na kuwatoroka uwanjani hapo.
Hayo yalibainishwa jana jijini humu na baadhi ya washiriki wa semina ya taratibu za usafirishaji na uingizaji madini, iliyoandaliwa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
Akichangia mada kuhusu biashara haramu na utoroshaji madini nchini, mmoja wa maofisa Usalama kwenye uwanja huo (jina tunalo), alisema utoroshaji madini hufanywa mara nyingi usiku kwa kuwa hakuna wakaguzi wa madini nyakati hizo.
Alisema, mara kadhaa wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi hasa usiku, upande wa ukaguzi wa abiria na mizigo, baadhi ya abiria huwa na nyara za serikali yakiwamo madini.
Abiria hao ambao wengine ni wafanyabiashara, kila wanapohojiwa juu ya vibali vya kusafirisha nyara hizo, huonesha nakala za vielelezo vya kuwaruhusu kufanya biashara hiyo.
Hata hivyo, aliongeza wanapowatilia shaka kwa kutaka uhakika wa nyaraka hizo, mara nyingi hukosa ushirikiano wa wakaguzi na wataalamu wa madini kwa muda huo na mara nyingi huacha abiria wakasafirisha madini hayo.
“Kuna changamoto kwenye eneo hili pale uwanjani hasa muda wa kazi wa watumishi wa umma unapokwisha, yaani baada ya saa 10 jioni, hakuna mtaalamu wa madini ambaye atakagua mizigo au kuhakiki nyaraka za kusafirisha madini hayo kwa abiria wa ndege za usiku,” alisema mtoa habari.
Alisema hali hiyo huwapa mwanya wafanyabiashara na abiria wengine kutorosha madini, kwa kuwa wanajua wataalamu wa ukaguzi wa nyaraka na vibali vya madini, hawapo nyakati hizo.
“Tunawakamata wengi bila vibali vya kusafirisha madini, tunawapeleka ofisi ya Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) uwanjani hapo, nao huwazuia kusafiri na huwaacha na kuwataka wakatafute vibali,” alisema mtoa habari.
Akisimulia mbinu chafu za baadhi ya wafanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, mtoa habari alisema kutokuwapo wakaguzi wa madini JNIA, kumesababisha mtandao feki wa wafanyabiashara wanaouza madini bandia kwa wageni.
Baadhi ya wafanyabiashara walio kwenye mtandao huo ni pamoja na mfanyabiashara maarufu wa jijini ambaye hivi sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji.
Kwa mujibu wa mtoa habari, wanunuzi wa madini hayo wanapobaini kwamba wameibiwa, huwaonesha maofisa usalama picha za wafanyabiashara hao.
“Unajua, pale uwanjani kuna mchezo unafanywa, kwa kweli maofisa madini wanahitajika wawepo saa 24, watawasaidia hata hao wanaoibiwa.
“Baadhi ya wageni wanaonunua madini kwa wafanyabiashara hao, huyakagua na kuhakiki kama ni madini halisi na hufikia makubaliano na kulipa malipo ya awali, kisha malipo mengine hufanyika wanapofika nchi zao,” alisema mtoa habari na kuongeza:
“Wakati wa makubaliano hayo, huingia mikataba na kuweka sili kwenye mizigo na wanapofika uwanjani tayari kwa safari, wafanyabiashara hao maarufu huwapa nyaraka bandia zinazoonesha wanasafiri pamoja,” alisema.
Alifafanua, kuwa matapeli hao hushawishi wanunuzi watangulie ndani ya uwanja kwa ajili ya ukaguzi na wao hujidai kupeleka mzigo upande wa pili kwenye ndege za mizigo.
“Lakini kumbe ndio wanawatapeli na kutokomea na madini hayo ambayo hata hivyo tayari huwa wameshachukua malipo ya awali,” alisema.
Mtoa habari huyo alisema wanunuzi hao wakiwa ndani ya uwanja, husubiri wauzaji wanaosafiri nao na wanapoona hawatokei, huenda kwao kuomba msaada kwa kuwaonesha picha za wafanyabiashara hao ambao huwapiga mapema wakati wakifanya makubaliano bila wao kutambua.
“Wanapogundua wameibiwa, huja kwetu kuomba msaada na hutuonesha picha kwenye kamera ambazo huwapiga wafanyabiashara hao bila wao kujua, na sura tunazooneshwa ni za baadhi ya wafanyabiashara maarufu, tunachoweza kuwasaidia ni kuwaambia waripoti Polisi,” alisema mtoa habari.
Aliongeza, kama wakaguzi wangekuwapo na kutumia Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, ambayo inakataza mtu asiye na leseni halali ya madini, kumiliki, kusafirisha au kuuza madini bila kibali cha kufanya hivyo, wangewakamata wengi na adhabu zingechukuliwa dhidi yao kama sheria inavyosema.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu anayekwenda kinyume na sheria, adhabu yake ni faini ya Sh milioni 10 au kifungo cha miaka isiyozidi mitatu jela au adhabu zote kwa pamoja.
Aidha, sheria hiyo inampa mamlaka Kamishna wa Madini kutaifisha madini yaliyokamatwa kinyume cha sheria, pamoja na vifaa vilivyotumika kuzalisha madini hayo.
“Sisi pale uwanjani hatulali, tunaingia kazini kwa shifti, sasa Wizara (ya Nishati na Madini) nayo ijipange walete vijana wachapa kazi wafanye kazi saa 24, kwani ndege zinaingia na kuondoka muda wote,” alisema mtoa habari.
Akijibu hoja hiyo na nyingine, Meneja Uthamini wa Madini wa TMAA, George Kaseza alisema hizo ni changamoto ambazo hatua zimeanza kuchukuliwa, kwa kuomba ushirikiano na wadau wengine ili kudhibiti wizi huo.
Kaseza alisema mkakati wa sasa ni kuendelea kuongeza madawati ya TMAA yenye wakaguzi kwenye maeneo yote ya vizuizi barabarani, mipakani na kwenye viwanja vya ndege ili kudhibiti utoroshaji madini nchini.