MWANAFUNZI ABAKWA NA WENZAKE DARASANI MBELE YA MWALIMU...

Darasa mbamo mwanafunzi huyo alimobakwa na wenzake.
Msichana mwenye miaka 15 mkazi wa New York amebakwa vibaya wakati aliponaswa sambamba na wavulana wawili pamoja na mwalimu wake aliyekuwa umbali wa hatua moja kutoka hapo, madai hayo yapo kwenye hati ya mashitaka yaliyofunguliwa Ijumaa.
Mwanafunzi huyo mwenye mahitaji maalumu, ametambulishwa tu kwa vifupisho K.J., amedaiwa kudhalilishwa kijinsia kwa dakika 10 huku mwanafunzi mwingine 'akimpiga kichwani kila alipokuwa akijaribu kutoroka,' wakati wa kipindi cha somo la sayansi katika Shule ya Martin De Porres mjini Elmont, New York.
Mama wa msichana huyo, ambaye amefungua mashitaka hayo, alidai kwamba mwalimu huyo alipuuzia shambulio hilo licha ya mwanafunzi mmoja kuwa akicheza juu ya dawati wakati mwenzake akiendeleza harakati za kumbaka K.J.
Japo msichana huyo aliwaeleza wafanyakazi wa shule hiyo siku iliyofuata, maofisa hao wa shule walishindwa kuripoti uhalifu huo.
K.J. ana ufahamu wa 60 na kwamba alipelekwa na Jiji katika shule hiyo ya De Porres.
Alikuwa ni msichana pekee katika darasa lenye wavulana 13.
Watuhumiwa wake wa shambulio hilo wote wamekuwa wakifahamika kwa 'matukio ya vurugu' na ni wakazi wa Casa De La Salle, eneo mashuhuri kwa uhalifu wa vijana.
Mama wa K.J. alisema hana uwezo wa kumfanyia uhamisho wa haraka binti yake, na ndio sababu ya msichana huyo kufanyiwa uonevu kwa miezi sasa.
Desemba, maofisa wa shule walimweka binti huyo kwenye chumba na mmoja wa wavulana ambaye amekuwa akimlazimisha kufanya naye mapenzi na kuwaasa 'kujadili masuala yao.'
K.J. alitoka kwenye shumba hicho akiwa na jeraha kubwa juu ya jicho lake la kulia.
"Inasumbua akili jinsi hili linavyoweza kutokea," mwanasheria Madeline Bryer alilieleza gazeti la the New York Post.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Ed Dana alisema uchunguzi wa ndani umeanza mara tu baada ya kusikika udhalilishaji huo na kumfukuza mwalimu huyo.
"Tunataka jamii ifahamu kwamba hivyo ndivyo tunavyowadhibiti walimu wetu katika viwango vya juu. Kipaumbele chetu cha juu kabisa ni usalama na uwepo wa wanafunzi katika uangalizi wetu," alisema Dana katika taarifa yake.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item