NDEGE YA ATCL YAPASUKA KIOO CHA MBELE, YATUA KWA DHARURA...

Zaidi ya abiria 25 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya ndege aina ya Bombardier Dash 8-300 waliyokuwa wakisafiria kupata hitilafu ikiwa angani na hivyo kumlazimu rubani wake kuirudisha ndege na kutua kwa dharura mkoani hapa.
Hayo yamethibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro, huku akiwataka wasafiri kutokuwana na hofu.
Hali hiyo imetokana na moja ya vioo vya mbele vya ndege hiyo kupasuka na hivyo kuruhusu upepo mkali kuingia ndani na hivyo kuwafanya marubani wa ndege hiyo kufanya kazi ya ziada kuhakikisha ndege hiyo inatua salama.
Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari yake ya kwanza mkoani humo ikiwa ni miezi 10 baada ya ndege nyingine ya shirika hilo kuanguka na kuharibika mkoani Kigoma.
Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo Athumani Batumwa na Fred Mbassa, walisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ilipata hitilafu ya kioo cha mbele kiasi cha dakika 30 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kigoma.
Kapteni Lazaro amekiri kutokea kwa hitilafu hiyo na amewaondoa hofu wasafiri juu ta tatizo hilo na kwamba ni sehemu ya matatizo yanayoweza kutokea kwa ndege yoyote.
Alisema kuwa utaratibu unafanywa kuhakikisha abiria waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo wanatafutiwa ndege nyingine ya kuwasafirisha hadi Dar es Salaam na kwamba hadi kufikia jana, abiria hao wangekuwa wameshatafutiwa ufumbuzi.
Hata hivyo, ndege ya ATCL inaweza kuanza kufanyiwa marekebisho kuanzia leo baada ya kuwasili kwa vipuri.
Hii ni mara ya pili kwa ndege ya ATCL mkoani Kigoma kupata hitilafu ikiwa inaelekea Dar es salama ambapo mapema mwaka jana moja ya ndege kampuni hiyo ilishindwa kuruka na hivyo kuserereka ambapo hadi sasa ipo kama chuma chakavu pembezoni mwa uwanja wa ndege mkoani hapa.

Post a Comment

  1. when will people learn to publish accurate information? this is an old pic of the plane that crashed in feb2012, the plane which had a mishap in kigoma was landed safely

    ReplyDelete

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item