NDOA BADO YAMTAFUNA "MAMA KIJACHO" KIM KARDASHIAN...

Kanye West (kushoto), Kim Kardashian na Kris Humphries (kulia).
Mwimbaji Kim Kardashian hajapanga kufunga pingu za mzaisha na Kanye West kwa sasa lakini amechukizwa na kukatishwa tamaa kwamba Kris Humphries anamuweka katika sehemu ambayo anazaa na mtu mmoja wakati yuko kwenye ndoa na mwingine.
Vyanzo vilivyo karibu na Kim vimeeleza ... hajisikii kuhitaji kufunga ndoa na Kanye, licha ya kwamba amezaa naye mtoto. Lakini hataki kuwa ameolewa kisheria na Kris Humphries wakati akijifungua mtoto wake.
Vyanzo vya habari vimesema ... Kim anahisi Kris amekuwa "mwenye chuki na kulipiza kisasi" katika kudai talaka -- ambayo amekuwa akivutana naye kwa karibu mwaka na nusu -- bila sababu za msingi. Imeelezwa hakuna ushahidi wowote wa kimaandishi uliowasilishwa na pande hizo mbili unaoonesha kwamba Kim alimlaghai Kris wakati walipokubaliana kufunga ndoa.
Vyanzo vinavyofahamu sakata hilo vimesema ... watu wa upande wa Kris sasa wanamuasa kufikia muafaka na kuachana nalo. Lakini yeye amekuwa tatizo ... Pande zote sasa zimekumbana na gharama kubwa za kuwalipa wanasheria, na imeelezwa kwamba Kim anaamini nguvu kubwa ya changamoto za kisheria kutoka kwa Kris ni upuuzi na kwamba anamtaka kulipa fidia gharama za wanasheria wa Kim.
Endapo watashindwa kuafikiana, Jaji atapanga tarehe ya kesi mwezi ujao. Mwanasheria wa Kim, Laura Wasser, anakadiria kesi hiyo itachukua siku nzima. Mwanasheria wa Kris anafikiria itachukua takribani siku 5, sababu anataka kuweka kipindi cha moja kwa moja cha Televisheni kuhusu kesi hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item