POLISI WALIOMPUUZA ALIYEBAKWA WAFUKUZWA KAZI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/polisi-waliompuuza-aliyebakwa-wafukuzwa.html
Msichana aliyebakwa Jyoti kabla na baada ya shambulio (pichani kushoto). |
Polisi wanne wamefukuzwa kazi na mwingine kuhamishwa kituo kutokana na namna walivyoshughulikia kesi mpya ya kubakwa na kuuawa msichana wa miaka 21.
Sambamba na hilo, watuhumiwa watano waliombaka mwanafunzi wa udaktari na kusababisha kifo chake wiki mbili baadaye, wamefikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Katika ubakaji huo mpya, msichana aliyefanyiwa kitendo hicho ni mfanyakazi wa kiwanda kilichopo Noida nje kidogo ya Mji wa Delhi.
Alikuwa anarudi nyumbani usiku na ndipo alipobakwa na kuuawa. Baba yake alipokwenda kutoa taarifa Polisi usiku wa Ijumaa alijibiwa kuwa msichana huyo amekwenda kulala na mtu lakini siku ya pili yake mwili wake uliokotwa.
Hadi sasa watu wawili wamekamatwa na mwingine kukimbia waliohusika na ubakaji huo.
Kutokana na ubakaji huo, kumeamsha maandamano makubwa katika Mji wa Noida.
Katika hatua nyingine watuhumiwa watano waliombaka mwanafunzi wa udaktari katika basi na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara wamefikishwa mahakamani huku watu wakizuiwa kuwapiga picha.
Watuhumiwa hao ni Ram Singh na kaka yake Mukesh, Pawan Gupta, Vinay Sharma na Akshay Thakur. Mtuhumiwa wa sita ambaye ana miaka 17 anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Watoto.
Wakati kesi hiyo ikiwa mahakamani, inaelezwa kuwa ulinzi umekuwa mkali sana kutokana na tukio hilo kuvuta hisia za watu wengi India na duniani kote.
Waendesha mashitaka wanasema wana ushahidi mzito dhidi ya watuhumiwa hao na iwapo watakutwa na hatia watahukumiwa kifo.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendeshwa na kukamilika katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Desemba 16 mwaka jana mwanafunzi huyo akiwa na rafiki yake wa kiume alibakwa kwa muda wa saa moja ndani ya basi kabla ya kutupwa pembeni mwa barabara.
Kutokana na ubakaji huo akafanyiwa operesheni tatu na baadaye kupelekwa Singapore kwa matibabu zaidi lakini alipoteza maisha akiwa hospitalini.
Tangu wakati huo hadi sasa maandamano yamekuwa yakiendelea nchini India ambapo watu wanataka kuwekwe sheria kali dhidi ya wanaowanyanyasa wanawake.
Waandamanaji hao wamekuwa wakitaka mbali na mabadiliko ya sheria pia mabadiliko katika Jeshi la Polisi ambao wameonekana kushindwa kuwafungulia kesi wabakaji kadhaa.
Hadi sasa familia ya msichana huyo haijawa tayari kuruhusu jina la msichana huyo aliyebakwa litolewe hadharani.
Hata hivyo Waziri Mkuu, Shashi Tharoon ameomba jina hilo liwekwe wazi ili litumike katika sheria mpya ya kupambana na ubakaji. Kwa sasa anatajwa kama XYZ.