NAHODHA WA BOTI ILIYOZAMA ZIWA TANGANYIKA KORTINI KWA MAUAJI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/nahodha-wa-boti-iliyozama-ziwa.html
Sehemu ya Ziwa Tanganyika. |
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Emanuel Mrangu, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Asiago Ocheng alidai Januari 3 mwaka huu katika Kijiji cha Herembe Wilaya ya Uvinza washitakiwa walimuua Wamjini Hussein; kosa ambalo limedaiwa ni kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 12.
Walisomewa pia mashitaka ya kumuua Nondo Iddi, Shani Baba, Muzinga Kandoro, Sara Joseph na Asha Hamisi.
Washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. Wamerudishwa rumande hadi Januari 21 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.
Wakati huo huo miili ya watu wanne waliozama katika boti hiyo imeonekana na kufanya idadi ya miili iliyopatikana kufikia 13.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Fraiser Kashai aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kwamba polisi na vikosi vingine vya uokoaji vinaendelea kutafuta miili ya watu wengine wanane ambayo haijapatikana hadi sasa.
Boti ya Yarabi Tunuru ilipata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita katika kijiji cha Herembe Wilaya ya Uvinza ikiwa njiani kutoka Wilaya ya Nkasi kwenda nchini Burundi ikiwa imebeba abiria 85 na tani 45 za mizigo.