SHEHENA YA NYARA ZA SERIKALI YAKAMATWA...

Kamanda Liberatus Sabas.
Polisi jijini hapa imekamata shehena ya nyara za Serikali zenye thamani ya mamilioni  ya fedha zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye makasha maalumu kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje.
Nyara hizo ni pamoja na mafuvu  ya simba, mamba, tembo na wanyama wa aina mbalimbali wa porini  na ngozi za chui, tembo, mamba na meno mawili ya tembo.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio Ngaramtoni ya Chini  jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas alisema nyara hizo zilikamatwa juzi usiku saa 3 asubuhi eneo la Mateves ambapo polisi walipewa taarifa kuwa Peter Laurence (55) alikuwa akihifadhi nyara hizo katika eneo la kiwanja chake.
Alisema baada ya polisi kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kukuta nyara hizo zikiwa zimehifadhiwa kwenye makasha huku kukiwa na mafuvu ya wanyama mbalimbali na ngozi za kondoo.
Alisema baada ya kuzikamata walimwuliza Laurence kama ana kibali lakini alisema kibali halisi alikuwa nacho ila kilipotea ingawa nyumbani kwake ana nakala ya vibali vya wanyama hao.
“Polisi kwa kushirikiana na watu wa Maliasili tunafanya uchunguzi kujua inakuwaje mtu huyo  kuwa na nyara hizi tangu mwaka 2007 hadi leo na kwa nini aziweke katika makasha na alikuwa akishirikiana na akina nani pia  kama zina vibali au la,” alisema Kamanda.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item