WAHUNI WATANO WALIOMBAKA MWANAFUNZI WASHITAKIWA KWA MAUAJI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/wahuni-watano-waliombaka-mwanafunzi.html
Wanawake wakiomboleza kifo cha mwanafunzi huyo aliyebakwa kwenye basi na wahuni. |
Wanaume watano wanaotuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa chuo kikuu kwa masaa kadhaa ndani ya basi lililokuwa likipita kwenye mji mkuu wa India wameshitakiwa kwa mauaji, ubakaji na mashitaka mengine ambayo yanaweza kuwatupa kwenye adhabu ya kifo.
Shambulio hilo dhidi ya binti wa miaka 23, ambaye alifariki kutokana na majeraha makubwa ndani ya mwili wake mwishoni mwa wiki iliyopita, limechochea mdahalo mkubwa nchini kote India kuhusu udhalilishaji wa wanawake na kuibua maandamano kila siku kutaka hatua zichukuliwe.
Kumekuwa na dalili za mabadiliko tangu kutokea shambulio hilo. Ubakaji, umekuwa ukipuuzwa, sasa ni habari kubwa katika kurasa za mbele, wanasiasa wametaka sheria kali zaidi, ikiwamo adhabu ya kifo na kemikali ya kuwahathinisha wabakaji, na serikali inachunguza kwa upana mabadiliko katika mfumo wa hukumu za makosa ya jinai dhidi ya vitendo vya ubakaji. Wanahatakati wanasema janga hilo linaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwa haki za wanawake.
Katika taifa ambako kesi mahakamani zinaweza kukaa kwa miaka, serikali imeanzisha mahakama maalumu Jumatano kushughulikia makosa dhidi ya wanawake, na kwamba ndiko mashitaka dhidi ya watuhumiwa hao watano yalikopelekwa Alhamisi jioni. Serikali hiyo ilisema inapanga kufungua mahakama nyingine nne zaidi kama hizo katika jiji hilo.
Mwendesha mashitaka Rajiv Mohan amefungua kesi ya ubakaji, kughushi ushahidi, kuteka nyara, mauaji na mashitaka mengine dhidi ya watu hao. Hati ya mashitaka haikuwekwa hadharani na alitaka mashitaka ya siri. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Jumamosi.
Watu hao walioshitakiwa ni Ram Singh, dereva wa basi hilo; kaka yake Mukesh Singh, mfagizi wa basi katika kampuni hiyo hiyo; Pavan Gupta, muuza matunda; Akshay Singh, mwosha basi; na Vinay Sharma, mkufunzi wa viungo. Hakuwapo mahakamani. Mamlaka zimesema zitashinikiza hukumu ya kifo kwa watu hao.
Baba wa binti mwathirika wa tukio hilo la ubakaji alisema anaunga mkono adhabu ya kifo.
"Hukumu ya nguvu na ya kuchukiza zaidi inatakiwa kutolewa," alisema, akiongeza kwamba anadhani sheria mpya zinatakiwa kutangazwa kufuatia binti yake.
Mtuhumiwa wa sita, aliyeorodheshwa kuwa na miaka 17, alikuwa akitarajiwa kuhukumiwa kwenye mahakama ya watoto, ambako hukumu yake ya juu inaweza kuwa kifungo cha miaka mitatu katika sehemu ya kurekebisha tabia. Polisi pia wanamshikilia mmiliki wa basi kwa madai kwamba alitumia nyaraka zisizo halali kuendesha huduma binafsi ya basi.
Umoja wa Mawakili ulisema wanasheria hawatatetea watuhumiwa kwa sababu ya aina ya mashitaka, lakini mahakama hiyo ilikuwa ikitarajiwa kuwateua wanasheria kuwatetea watuhumiwa hao.
"Adhabu kali, kali, kali lazima itolewe kwao," alisema Ashima Sharma, mwanafunzi mwenye miaka 18 aliyehudhuria maandamano Alhamisi. "Adhabu kali mno ... kwamba wanaume wote India lazima wafahamu hawatawatendea wanawake kama walivyokuwa wakiwafanyia."
Msichana huyo alishambuliwa Desemba 16, mwaka jana baada ya kupanda basi akiwa ameambatana na mwanaume baada ya kutoka kutazama onesho la jioni la filamu ya "Life of Pi" kwenye jengo moja. Gari hilo lilikuwa basi la abiria ambalo liliwachukua abiria hao wawili kinyume cha sheria, mamlaka zilisema.
Wawili hao walishambuliwa kwa masaa ndani ya basi hilo lililokuwa likikatiza jijini humo na wakati mwingine kupita vituo vya ukaguzi vya polisi wakati wa shambulio hilo. Hatimaye walitoswa wakiwa watupu kando ya barabara. Msichana huyo, ambaye jina lake halikutajwa, alishambuliwa kwa kutumia nondo na kupata majeraha makubwa ya ndani ambapo yalithibitishwa kuwa yanahatarisha maisha yake.
Nje ya mahakama, wanasheria wanawake wapatao 50 waliandamana, wakitaka mabadiliko makubwa ya mfumo wa hukumu za makosa ya jinai kuhakikisha haki kwa wanawake. "Adhibu polisi, amsha mahakama, komesha ubakaji," lilisomeka moja ya mabango ya waandamanaji.