WATAALAMU WA KIGENI SASA CHAGUO LA PILI AJIRA TANZANIA...

Balozi Ombeni Sefue.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuwa kuanzia sasa itawatumia zaidi wataalamu wa Kitanzania, walioko ndani na nje ya nchi, katika kutekeleza mipango yake yenye umuhimu wa kitaifa.
Hayo yamo katika taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kwa vyombo vya habari.
Katika taarifa yake, Balozi Sefue anasema  chini ya mpango huo, wataalamu wa nje watatumika tu pale ambako wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi, hawatapatikana kufanya kazi husika.
Awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine wakipewa chaguo la kwanza lakini sasa lengo ni kutumiwa kwa wataalamu Watanzania.
Katika utekelezaji wa uamuzi huo, Serikali imetangaza kutafuta wataalamu wa Kitanzania kwenye maeneo ya mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesiasilia na mafuta.
Aidha, inawatafuta wataalamu wake katika Teknolojia ya Habari ya Mawasiliano (Teknohama) kwa lengo la kuimarisha matumizi salama ya Teknohama katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pia inawatafuta wataalamu watakaosaidia kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha nchi inapata matokeo makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.
Katika taarifa hiyo, Balozi Sefue amesema wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo hayo watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo utendaji wao utaridhisha.
“Kutokana na uamuzi huo Serikali sasa inatoa mwito kwa wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ndani ya nchi ama ughaibuni, kujitokeza na kutuma wasifu wao pamoja na maeneo ya kwa nini wanafikiri wao ni aina ya watu ambao wanahitaji kuifanya kazi hiyo ya Serikali,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item