ABIRIA WENYE UZITO MKUBWA KUPANDISHIWA NAULI KWENYE NDEGE...

Abiria wenye uzito mdogo sasa wanaweza kupewa punguzo kubwa la nauli.
Mpango wa kulipa kadri ya uzito ulionao kwenye ndege unaweza kuanza kutumika sababu watu wenye uzito mkubwa wanagharimu zaidi katika mafuta wakati wa kuruka, profesa mmoja amedai.


Abiria wazito zaidi watalipa zaidi kwa ajili ya tiketi zao za ndege na wale wepesi watapunguziwa chini ya mipango iliyowasilishwa na Dk Bharat P Bhatta.
Akiandika kwenye chapisho lake la kila mwezi la Journal of Revenue and Pricing Management, Dk Bhatta alisema uzito na nafasi lazima vitazamwe kwa makini wakati mashirika ya ndege yanapopanga nauli.
Dk Bhatta, kutoka Chuo cha Sogn go Fjordane nchini Norway, alisema: "Kutoza kutokana na uzito na nafasi ni kanuni inayokubalika kabisa, sio tu kwenye usafirishaji, lakini pia katika huduma nyingine.
"Huku uzito na nafasi vikiwa ni muhimu katika usafiri wa anga kuliko njia nyingine za usafiri, mashirika ya ndege yanatakiwa kufanyia kazi hili wakati wanapopanga nauli zao."
Mhariri wa Journal of Revenue and Pricing Management, Dk Ian Yeoman alisema: "Kwa mashirika ya ndege, kila kilo inayozidi inamaanisha gharama zaidi ya mafuta lazima yachomwe, ambayo inapelekea gharama za kifedha.
"Wakati biashara ya mashirika ya ndege ikikumbwa na matatizo ya kifedha, faida kiduchu na kushuhudia ukuaji mdogo katika karne iliyopita, pengine watalazimika kujiandaa kuweka mizani katika sehemu za ukaguzi wa abiria."
Dk Bhatta anasema nauli inaweza kuwekwa vya kudumu kwa kilo kwa abiria hivyo kwamba mtu mwenye uzito wa kilo 60 analipa nusu ya nauli ya ndege ya mtu mwenye kilo 120.
Mbadala wake, mashirika ya ndege yanaweza kuwa na nauli 'ya kuanzia' sambamba na gharama za ziada kwa abiria wazito kufidia gharama za ziada, pamoja na punguzo kwa abiria wenye uzito mdogo.
Mapendekezo hayo yana mkashifishaji, kama Bob Atkinson wa TravelSupermarket.com. Alihoji kama abiria watastahili punguzo kama wanapungua uzito katikati wakati wanakata tiketi zao na wakati wanawasili kwenye uwanja wa ndege.
Alieleza: "Wateja tayari wameshalipa gharama za ziada kwa ajili ya mizigo yao, lakini wanaongeza moja kwa mtu - nafikiri hiyo ni kiasi fulani cha maudhi."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item