ALIYEMUIBUA "THE UNDERTAKER" MIELEKA YA WWE AFARIKI DUNIA...

William Moody maarufu kama Paul Bearer.
Paul Bearer -- meneja wa kutisha wa WWE ambaye alisaidia kumtambulisha The Undertaker katika ulimwengu wa mieleka -- amefariki dunia juzi jioni akiwa na umri wa miaka 58 ... hii ni kwa mujibu wa WWE.
Bearer -- ambaye jina lake halisi ni William "Bill" Moody -- alijiunga na WWE mwaka 1990 alichukua jukumu la umeneja akiwasimamia nyota kadhaa wa mieleka wakiwamo Undertaker, Kane, Rick Rude, Vader na Mankind.
Taarifa kuhusiana na kifo cha Bearer hazijafahamika -- lakini aliripotiwa kusumbuliwa na matatizo makubwa ya kiafya kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita ... ikiwamo unene uliokithiri na tishu za kibofu.
WWE limetoa taarifa ikisema ... "WWE imehuzunishwa kupata taarifa za kifo cha William Moody, maarufu kama Paul Bearer."
"Moody alianza majukumu yake katika mieleka ya WWE mwaka 1991 kama meneja wa Undertaker na aliendelea hadi kufikia kuwa kiungo cha kukumbukwa ya WWE katika kipindi cha miaka 20 iliyofuata. Salamu zetu za rambirambi ziende kwa familia ya Moody, marafiki na mashabiki wake."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item