TAASISI YA MOI KUANZA UPASUAJI WA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA...

https://roztoday.blogspot.com/2013/03/taasisi-ya-moi-kuanza-upasuaji-wa.html
![]() |
Wataalamu wa Upasuaji MOI wakiwa kazini. |
Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) inatarajiwa kuanza kufanya upasuaji kwa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa baada ya kupatiwa msaada wa vifaa vya upasuaji kutoka Saudi Arabia.
Msaada huo wa vifaa vya matibabu vyenye thamani ya Dola za Marekani milioni 140, ulikabidhiwa kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Monimal.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni: vya kusaidia kupumua wakati wa upasuaji, vifaa vya ultra sound na mashine za nusu kaputi.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, Mwinyi alisema vifaa hivyo vitasaidia MOI kuanza kufanya upasuaji huo, kwani kila mwaka watoto zaidi ya 4,000 huzaliwa wakiwa na matatizo hayo na nusu yao pekee ndiyo wanapata matibabu.
Alisema msaada huo umepatikana kwa jitihada za Menejimenti ya MOI na Chama cha Wazazi wa Watoto wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo wazi (ASBAHT), ambao walipeleka maombi katika nchi hiyo ili kupatiwa vifaa.
Alisema licha ya juhudi mbalimbali, watoto wengi hawapati matibabu ya ugonjwa huo, kutokana na wengi wao kufika hospitali wakiwa wamechelewa, kutokana na umasikini na matatizo mbalimbali ya kifamilia.
Dk Mwinyi alimshukuru Balozi huyo, kwa kumweleza kuwa misaada hiyo itaongeza hamasa ya wazazi wengi kupeleka watoto wao kutibiwa, ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya watoto hao.
Alisema Tanzania na Saudi Arabia zipo katika mazungumzo kujenga wodi kwa ajili ya watoto hao ili kuhakikisha wanapata matibabu ipasavyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa ASBAHT , Dk Tares Al-Arnoos alishukuru kwa msaada huo, utakaosaidia kutibu watoto hao, ambao idadi yao inazidi kuongezeka kila mwaka.