ALIYETUMIKIA MIAKA 23 JELA KIMAKOSA AACHIWA HURU, APATA MARADHI YA MOYO...

David Ranta (katikati) akitoka gerezani.
Mtu ambaye aliachiwa huru baada ya kutumikia miaka 23 jela kwa makosa ambayo hakufanya anasumbuliwa na shambulio kubwa la moyo siku moja baada ya kuachiwa kwake.
David Ranta alikimbizwa hospitali ya New York Ijumaa usiku ambako aligundulika kwamba mmoja wa mishipa yake ya damu kuwa umeziba kabisa na mwingine ukiwa umeziba kidogo.
Mwanasheria wa Ranta, Pierre Sussman, alisema kwamba mteja wake alipokea matibabu na atalazimika kufanyiwa upasuaji mwingine.
Mlevi wa dawa za kulevya asiye na ajira, Ranta alihukumiwa kifungo cha miaka 37 na nusu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Rabbi Chaskel Werzberger mjini Williamsburg mnamo Februari 8, 1990.
Ranta aliachiwa huru Alhamisi baada ya majaji kugeuza hatia yake, ambayo ilipatikana kwa ushahidi wa uongo na kuweka wazi kwamba ulipotoshwa na polisi.
Mtu huyo mpya huru alikuwa akiishi kwenye hoteli na familia yake kufuatia kuachiwa kwake huku akiingia katika maisha yake mapya baada ya kutumikia karibu robo ya karne ndani ya gereza lenye ulinzi mkali.
Ijumaa usiku, mtu huyo mwenye miaka 58 alihisi maumivu mgongoni mwake na mabegani na kuwa na joto kali, kwa mujibu wa Sussman.
Kwanza, wapendwa wa Ranta walifikiri alipatwa na shambulio la mchecheto, lakini muda mfupi baadaye wakabaini kwamba ni mbaya zaidi ya hayo.
"Kiasi cha miaka yake katika gereza ambayo David ametumikia ni kitu kikubwa," aliongeza Sussman.
Shuhuda mtoto, ambaye ushahidi wake ulimtupa mwanaume huyo miaka 23 jela kwa mauaji ya mwalimu wa New York ambayo hakutenda, amezungumzia jinsi polisi walivyomweleza kumtambua mtu ambaye ametuhumiwa kimakosa.
Menachem Lieberman alikuwa na umri wa miaka 13 wakati alipooneshwa mstari wa watuhumiwa wa mauaji ya mwalimu wa dini ya Kiyahudi Chaskel Werzberger katika wizi wa almasi ambao haukufanikiwa.
Uamuzi wake wa kuhifadhi taarifa yake ulisababisha kuachiwa kwa David Ranta aliyetiwa hatiani kimakosa kutoka katika gereza lenye ulinzi mkali juzi baada ya miaka 23 ya kufungiwa humo.
Ranta aliachiwa huru baada ya jaji kupindua hatia yake ambayo ilisukumwa na ushahidi wa kimakosa wa shuhuda na mstari uliotengenezwa na polisi.
Sasa akiishi Montreal, shahidi huyo mwenye miaka 36 juzi alieleza jinsi polisi walivyomweleza kumchagua Ranta wakisema lazima 'achague yule mwenye pua kubwa'.
Mlevi wa dawa za kulevya asiye na ajira Ranta alihukumiwa kifungo cha miaka 37 na nusu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwalimu wa dini ya Kiyahudi Chaskel huko Williamsburg mnamo Februari 8, 1990.
Siku hiyo mtu mmopja alijaribu kuteka gari lenye almasi na pale iliposhindikana kuliteka gari la mwalimu wa dini ya Kiyahudi Chaskel - alimpiga risasi kisogoni na kumuua.
Mauaji hayo yamebwatisha jamii ya Kiyahudi ya Kihasidi mjini Brooklyn na kutaka adhabu kali kwa aliyehusika.
Akiwa bado mwanafunzi wakati huyo, Lieberman alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kutoroka kwa mtu huyo na utambulisho chanya wa Ranta ulishuhudia akifungwa mwaka 1991.
Zaidi ya miaka aligundua kwamba chaguo lake ulishinikizwa na mwaka 2011 - miaka 20 baadaye - aliamua kushirikisha wengine mashaka yake yote hayo.
"Huku miaka ikisonga, nilikumbuka mtu fulani aliniambia," alisema. "Kadri nilivyokuwa nikiona taarifa za kuachiwa kwa watu wasio na hatia - nilianza kufikiria nyuma hukumu ambayo nilihusishwa," alifafanua.
"Sikumweleza yeyote katika hii dunia lakini nilivyokuwa nikiendelea kukua na kuona zaidi na zaidi ya hizi hatia za kimakosa hakika ilinisumbua. Miaka miwili iliyopita nikaamua lazima nilitoe kifuani kwangu.
"Mtu asiye na hatia alikuwa jela na sasa ameachiwa huru - sehemu ya huzuni ni kwamba muuaji hajahukumiwa. Najihisi nilipangwa kama mtoto na nilitaka tu kutekeleza sehemu yangu katika hukumu."
Mpelelezi katika kesi hiyo, Louis Scarcella bado anapinga makosa yoyote na anasema hakukuwa na jaribio lolote la kumkomoa Ranta.
Hatahivyo, matatizo mengine yaligunduliwa pale Kitengo cha Uadilifu wa Hatia kilipotazama kesi hiyo.
Karatasi ziligundulika kupotea na miongozo mingine ikionekana kuwa haikuchunguzwa.
Mtuhumiwa mkuu mwingine alikuwa mlevi wa dawa za kulevya Joseph Astin. Mkewe alichunguzwa mwaka 1996 alikiri mauaji shidi yake siku hiyo lakini alifariki miezi miwili baadaye.
Katika yote, hii ilishawishi mahakama hiyo kwamba ulikuwa muafaka wa kumwachia Ranta, baba wa watoto watatu mwenye miaka 58.
Ndugu, akiwamo binti yake mdogo ambaye alikuwa mtoto mchanga wakati alipohukumiwa kifungo, walibubujikwa machozi na kupiga kelele za furaha.
Mwalimu wa dini ya Kiyahudi, Chaskel alikuwa kipendwa mno na wafuasi wake wa jumuiya ya Brooklyn.
Maelfu ya watu walihudhuria mazishi yake, na Meya wa wakati huo David Dinkins alitangaza dau la Dola za Marekani 10,000 kwa yeyote aliyekuwa na taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa.
Wakati Ranta alipokamatwa, gari la polisi lililomchukua kumpeleka jela lilizingirwa na wati wakiimba, "Hukumu ya kifo!"

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item