AUA MWANAE KWA RISASI WAKATI AKISAFISHA BUNDUKI SEBULENI...

Mtoto Christopher Stanlane Jr.
Mtu mmoja wa North Carolina kwa bahati mbaya amempiga risasi na kumuua mtoto wake wa kiume mwenye miaka 10 wakati alipokuwa akisafisha bunduki yake kwenye sebule yao.
Imeelezwa kwamba Christopher Stanlane mwenye miaka 34 alikuwa kwenye kochi nyumbani kwake Fairmont akifuta vumbi katika silaha yake ndipo ikafyatuka risasi majira ya Saa 10 jioni ya Jumapili.
Mtoto wake Christopher Stanlane, Jr., alikuwa akitazama runinga mbele yake wakati risasi ilipofyatuka, Kapteni Anthony Thompson alisema, na risasi ikampiga mvulana huyo kisogoni.
"Alikuwa makini sana na silaha hiyo," alisema Robert Simmons, mjomba wa mtoto huyo. "Sifikirii kabisa kama alidhamiria kuelekeza upande ule. Lazima kulikuwa na risasi imewekwa kwenye chemba na ilifyatuka na kumpiga."
Baba huyo alitupa bunduki yake na kumkimbilia binti yake wa miaka minane aliyekuwa kwenye chumba kingine.
Mkewe, ambaye alikuwa akiandaa chakula cha usiku wakati janga hilo likitokea, alipiga simu polisi. Madaktari waliwasili nyumbani hapo na kutangaza kwamba mtoto huyo amefariki katika eneo la tukio.
Hakuna mashitaka yoyote yaliyofunguliwa kuhusiana na kesi hiyo.
Thompson anasema Wanasheria wa Wilaya ya Robeson County wataamua mara moja endapo mashitaka yoyote yatafunguliwa dhidi ya baba huyo.
Simmons alisema wazazi hao wamepata mshituko, wakijaribu kujua hasa nini kilichotokea.
Simmons alisema Christopher mdogo atakumbukwa mno na familia yake.
"Alikuwa mtoto mzuri. Alikuwa mshirika wangu. Hakuna neno zaidi la kusema kumwelezea jinsi tutakavyomkumbuka, ni tukio gumu sana kuaminika."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item