AUA MWANAE NZEGA! KISA? ETI KATOROKA SHULE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/aua-mwanae-nzega-kisa-eti-katoroka-shule.html
| Kamanda Anthony Rutta. |
Mkazi wa kata ya Kasela, kitongoji cha Njuka wilayani hapa, Asha Athumani (42) anatuhumiwa kumpiga mtoto wake hadi kumuua kutokana na utoro wa shule.
Akizungumza na mwandishi jana Diwani wa Kasela, Regina Nduru alidai kuwa tukio hilo limetokea Machi 6 saa moja usiku.
Diwani huyo alimtaja mtoto huyo kuwa ni Girode Gagi (11) ambaye alikuwa akisoma darasa la 4 shule ya msingi Lububu wilayani hapa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wajumbe wa Serikali ya Kijiji hicho ambao majina yao hawakutaka yaandikwe, walisema mtoto huyo alikuwa mtoro wa shule kwa nyakati tofauti shuleni hapo.
Waliendelea kudai kuwa mama huyo alimwadhibu mtoto huyo kwa kumfunga kamba mikononi na kumpiga hadi kusababisha kifo hicho.
Walisema tukio hilo lilipotokea, walipata taarifa kuwa mtoto huyo amefariki dunia huku akiwa na jeraha kubwa kichwani na alama za viboko miguuni.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Saidi Hassani, alisema taarifa kutoka kwa mama wa mtoto huyo zilisema alimpa adhabu akakimbia na kudondokea kitu chenye ncha kali na kuvuja damu nyingi na kumsababishia umauti.
Lakini Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, taarifa za utoro wa mtoto huyo zilikuwa bado hazijafika katika ofisi za kijiji ili kufanyiwa kazi.
Taarifa ya Mganga Mkuu wa zahanati ya Mwangoye mjini hapa, Sylvester Lutozi ilisema mwili wa Girode ulikutwa na jeraha kichwani likitoa damu nyingi hadi kusababisha kifo chake pamoja na uvimbe kisogoni uliotokana na kipigo.
Mtuhumiwa alifikishwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Mwangoye na kuachiwa huru, jambo ambalo baadhi ya wananchi walishindwa kulielewa kutokana na kutuhumiwa kwa kosa hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Anthony Rutta alisema taarifa kamili ya tukio hilo itatolewa baada ya kupata usahihi kutoka kwa watendaji wake.
Taarifa za kuachiwa huru kwa mtuhumiwa huyo zilithibitishwa na Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Njuka, Manyama Mabala akisema mtuhumiwa yuko huru kwa mujibu wa kaka wa mtuhumiwa ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Baadhi ya maofisa wa Polisi wilayani hapa walieleza kushangazwa kuachiwa kwa mtuhumiwa huyo bila upelelezi zaidi wa mauaji hayo kufanyika.
Maofisa hao ambao hawakupenda majina yao kuandikwa walidai kuwa mtoto huyo alipigwa na mama yake kwa fimbo ambayo awali ilifikishwa kituoni kwa ushahidi, lakini baadaye ilitoweka sambamba na mtuhumiwa huyo ambaye pia hakuchukuliwa maelezo wala kusajiliwa kwenye vitabu vya ofisi.