UHURU KENYATTA SASA NJIA NYEUPE KUINGIA IKULU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/uhuru-kenyatta-sasa-njia-nyeupe-kuingia.html
Wakati hadi jana usiku Uhuru Kenyatta akiwa anaongoza kwa kura 5,159,344 huku Raila Odinga akimfuatia kwa kupata kura 4,516,660, Mahakama Kuu nchini Kenya iliamua jana kwamba haina uwezo wa kusikiliza pingamizi lolote linalohusu uchaguzi wa Rais.
Uamuzi huo ulikuja kufuatia jaribio la kutaka kuzuia kazi ya kuhesabu kura kwa mikono.
Majaji Isaac Lenaola, Weldon Korir na David Majanja walitupilia mbali maombi ya dharura ya Kituo cha Utawala wa Wazi cha Afrika (AFRICOG) wakisema ingawa kikundi hicho kiliibua masuala mazito, bado hakiwezi kubatilisha mamlaka iliyonayo Mahakama hiyo.
“Masuala yaliyoibuliwa si madogo lakini yanatakiwa kushughulikiwa na chombo kinachostahili. Hatuna sababu ya kutaka kubaini kuwa tuna mamlaka ya kushughulikia suala hilo kwa sababu uchaguzi wa Rais si tukio moja bali ni mchakato,” walisema majaji hao katika uamuzi wao.
Mara tu baada ya uamuzi huo, kundi hilokupitia mwanashetia wake, Harun Ndubi lilisema litazinagtia maelekezo ya mahakama hiyuo na kuwasilisha maombi mengine katika Mahakama ya juu zaidi.
AFRICOG ilitaka kusimamisha kazi ya kuhesabu kura za urais kwa mikono ikidai kuwa tume ya uchaguzi na mipaka ilikuwa inakiuka vifungu vya JKatiba ambavyo vinataka iendeshe mchakato wa kuihesabu kura kwa uwazi zaidi.
Ndubi alisema kushindwa kwa tume hiyo kutumia vifaa vya elektroniki kuitangaza matokeo kumeathiri kabisa uhalali wa mchakato wa klutangaza matokeo.
“Tume hii inatumia mfumo wa kuhesabu kjura kwa mikono ki nyume na sheria na kupuuza ukweli kwamba idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika majimbo imebainika kuwa kubwa kuliko waliojiandikisha,” alisema Ndubi.
Majaji hao awali walishughulikia suala la kama wana mamlaka ya kuamua mngogoro huo. Ndubi hata hivyo alisema Mahakama Kuu ina mamlaka hiyo ya kusimamisha mchakato huo kwani nia yao haikuwa kupinga matokeo bali ni kufuata utaratibu ulioweklwa katika kutangaza matokeo hayo.
“Hapa hatupingi matokeo bali maombi yaliyowasilishwa kwa mujibu wa Kifungu 35 cha Katiba kuhusu Tume kushindwa kulinganisha na kuthibitisha kura vituoni,” alisema Ndubi.
Tume kupitia mwansheria wake, Paul Nyamodi ilipinga maombi hayo imkisema suala lolote linaloguisa uchaguzi wa urais linaachwa kwa Mahakama ya juuzaidi.
“Uchaguzi wa urais si tukio bali ni mchakato unaoshugvhulikia masuala ypote yanayotokea kuanzia uteuzi wa wagombea. Majaji hawa hawana budi kuachana na suala hili na kutupilia mbali maombi hayo au kuyapeleka katika mahakama inayohusika,” alisema Nyamodi.
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya yanatarajiwa kutangazwa muda wowote leo kutokana na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini humo kusema ilitarajia kukamilisha kazi ya kukusanya matokeo yote jana usiku wakati huo ikiwa imebakiwa na majimbo 30.
Mkurugenzi wa IEBC, Issack Hassan aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa majimbo 30 yalikuwa hayajahesabiwa na kuwataka Wakenya kuendelea kuwa watulivu wakisubiri kumalizia kuhesabu majimbo hayo.
Alisema changamoto zilizojitokeza katika kuhesabu kura zisiwe sababu ya kutomaliza uchaguzi huo salama, bali itumike kujifunza ili wakati mwingine yasitokee.
Akizungumza katika mkutano huo Hassan aliwashukuru Wakenya kwa uvumilivu walioonesha kutokana na matokeo kuchelewa tofauti na walivyotarajia.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo, James Oswago aliwaeleza Wakenya kuhusu njia ambayo Tume ilitumia kujumlisha matokeo ya uchaguzi wa urais.
Mjini Kisumu kwenye ngome ya Raila kulionekana kuwapo utulivu, huku watu wakirejea kazini, ingawa bei za bidhaa zilianza kupanda kutokana na wafanyabiashara kuhofia kwenda maeneo jirani kununua vyakula hadi matokeo yatakapotangazwa.