BABA WA GARY NA PHIL NEVILLE KORTINI KWA MADAI YA UBAKAJI...

Mzee Neville Neville (kushoto) akiwa na mwanae, Gary.
Nyota wa soka Gary na Phil Neville wanasemekana walipatwa na mshituko mkubwa usiku wa juzi baada ya baba yao kukamatwa kwa madai ya shambulio la aibu.
Neville Neville, mwenye miaka 63, alikuwa akishikiliwa mapema Jumamosi asubuhi baada ya mwanamke aliyejawa hofu kuwapigia simu polisi kufuatia madai ya tukio hilo.
Wakala huyo wa soka anaaminika kutoka Ijumaa usiku na kupata vinywaji na rafiki zake kwenye baa. Mwishoni mwa jioni hiyo mwanamke mmoja anadaiwa kumpa lifti baba huyo ya kwenda nyumbani kwenye gari lake.
Lakini mwanamke huyo anadai kwamba wakati akiendesha gari kumpeleka nyumbani kwake baba akamdhalilisha kijinsia.
Neville alikamatwa kwa tuhuma za shambulio la aibu kabla ya kuachiwa kwa dhamana hadi hapo atakapoitwa tena kujibu mashitaka dhidi yake.
Juzi usiku hakukuwa na majibu yoyote kutoka kwenye nyumba yake yenye thamani ya Pauni za Uingereza 650,000 anayoishi na mkewe, Jill, mwenye miaka 61, iliyoko North Manor, huko Bury. Majirani walikataa kutoa maoni yoyote.
Mtoto wa kiume wa Neville, Gary, mwenye miaka 38, mchezaji wa zamani wa Manchester United na nyota wa England, sasa ni mchambuzi wa soka kwenye televisheni ya Sky Sports. Phil Neville, mwenye miaka 36, bado anachezea timu ya Everton na alikuwa akichezea England. Dada yake pacha, Tracey alikuwa mchezaji netiboli wa England.
Chanzo cha habari za soka kilisema: "Gary na Phil wamefadhaishwa mno na radi hii.
"Maisha ya familia yao imara yamekuwa mwamba wakati walipojenga rekodi yao ya mafanikio hivyo madai haya yamekuja kuchafua kabisa rekodi hizo. Ni salama kusema wapo kwenye mshituko mkubwa. Neville na mkewe wanandoa wa aina yake na wanaonekana kuwa na ndoa imara."
Alicheza kriketi kwenye klabu ya Greenmount inayoshiriki Ligi ya Kriketi ya Bolton katika miaka ya 1980 kabla ya kuja kuwa mkurugenzi anayeheshimika wa timu ya soka ya Bury.
Neville alivutiwa na kuwashauri watoto wake wawili wa kiume na kufanya kazi kama wakala wao, wakiwawakilisha wote kwenye mazungumzo ya mikataba na klabu zao.
Juzi Polisi wa Greater Manchester walisema: "Polisi wanachunguza shambulio la aibu ambalo limetokea mapema Jumamosi asubuhi ya Machi 23, 2013 katika eneo la North Manor huko Bury. Mwanaume mwenye miaka 63 kutoka Bury alikamatwa kwa tuhuma za shambulio la aibu na amewekewa dhamana hadi Mei akisubiria kusomewa mashitaka."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item