MAHALI ATAKAPOZIKWA BILIONEA WA ARUSHA KUJULIKANA LEO...

Marehemu Nyaga Mawalla.
Familia ya marehemu Nyaga Mawalla, inatarajia kutoa taarifa rasmi ya wapi maziko ya bilionea huyo kijana, yatafanyika.
Mawalla alifariki wiki iliyopita nchini Kenya, katika Hospitali ya Nairobi alipokwenda kutibiwa ugonjwa wa moyo, uliokuwa ukimsumbua.
Akizungumza na mwandishi jana kwa njia ya simu, mmoja wa mawakili wa Kampuni ya Mawalla Group, Albert Msando, alisema familia imemaliza vikao vyake na leo, inatarajia kutoa taarifa ni lini mwili utaletwa, na wapi maziko ya bilionea huyo
yatafanyika.
Msando alisema taarifa zilizokuwa zikiandikwa katika vyombo mbalimbali, kuwa kuna mvutano katika suala la maziko, sio za kweli kwani kuna taratibu zinaandaliwa za maziko ambazo hata hivyo, hakuwa tayari kuzitaja.
"Fanyeni subira, kila kitu kitakuwa wazi kesho (leo) kuhusu wapi maziko yatafanyika, lini maiti itakuja nchini na hakuna malumbano juu ya hilo ndani ya familia," alisema Msando.
Hata hivyo Msando alikiri kuwa mwili wa marehemu Mawalla, bado uko Hospitali ya Nairobi na kusisitiza leo taarifa za mwili huo kuja nchini zitajulikana.
Marehemu Mawalla aliacha wosia kuwa atakapokufa, maziko yake yafanyike katika Kijiji cha Momela wilayani Arumeru, mkoani Arusha katika mashamba makubwa aliyowahi kununua jijini Arusha.
Pamoja na hilo, lakini mama yake mzazi ambaye jina lake halijapatikana, amesisitiza angependa mwanawe kipenzi azikwe nyumbani kwao Marangu Moshi, na sio mahali pengine popote.
Pia baba yake, Juma Mawalla, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa hatohudhuria mazishi ya mwanawe, iwapo atazikwa eneo tofauti na Marangu.
Taarifa zilisema kutokana na utata huo, vikao vya familia vinamsubiri mdogo wa marehemu, anayeshughulikia mwili Nairobi, aje kumaliza utata huo wa kifamilia.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item