BOBBY BROWN AJIPELEKA MWENYEWE GEREZANI...

Bobby Brown.
Bobby Brown amejikabidhi mwenyewe kwa mamlaka husika.

Mwimbaji huyo mwenye miaka 44 na mume wa zamani wa hayati Whitney Houston - ambaye alizaa naye binti Bobbi Kristina mwenye miaka 19, - alifungwa jela Los Angeles Jumatano asubuhi baada ya kuwa ameamriwa kujipeleka mwenyewe ndani kufuatia tukio la hivi karibuni la kuendesha gari huku akiwa amelewa ambalo lilimtia hatiani.
Bobby - ambaye pia ana watoto LaPrincia, Landon, Robert (Bobby) Brown Jr. na Cassius kwenye mahusiano mengine - alipandishwa kizimbani ndani ya chumba cha mahakama, ambako aliambatana na mwanasheria wake Tiffany Feder, kwa mujibu wa chanzo cha habari.
Bobby alihukumiwa kifungo cha siku 55 jela na miaka minne ya kuwa chini ya uangalizi mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kukamatwa na kushitakiwa kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa Oktoba, 2012 ikiwa ni mara ya tatu.
Mwimbaji huyo alikuwa chini ya uangalizi wakati huo kufuatia tukio la kuendesha huku akiwa amelewa Machi mwaka huu na alikuwa ameamriwa kuhudhuria mpango wa miezi 18 wa tiba ya pombe.
Baada ya kushindwa kutokea mahakamani katika tarehe aliyopangiwa mwezi uliopita mjini Los Angeles, ambako mwanasheria wake alimtetea kwamba 'hana hatia', nyota huyo wa miondoko ya R&B aliamriwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Alcohol Anonymous (AA) kwa wiki hadi siku ya kusikilizwa kwa shauri lake Jumatano.
Bobby na Whitney walitalikiana mwaka 2007 baada ya miaka 15 ya ndoa yao, ambayo hapo kabla Whitney aliielezea kama 'dhoruba' na iliyojazwa dawa za kulevya.
Mwimbaji huyo taswira alifariki dunia Februari, 2012 akiwa na umri wa miaka 28 kufuatia ajali ya kuzama kwenye chumba cha wageni kwenye Hoteli ya Beverly Hilton Hotel, mjini California.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item