HIZI NDIZO SABABU ZA PAPA MPYA KUCHAGUA JINA 'FRANCIS'...

Papa Francis I.
Papa Francis ametangaza waziwazi Jumamosi muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwake, akiwaeleza waandishi kwamba alivutiwa mara moja kuchukua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi sababu ya kazi yake kwa ajili ya amani na mafukara - na kwamba yeye mwenyewe angependa kuona 'kanisa fukara na kanisa kwa ajili ya mafukara."
"Wacha niwasimulie hadithi," Francis alisema katika mapumziko kwenye waraka wake ulioandaliwa wakati wa mkutano maalumu na maelfu ya waandishi wa habari, wafanyakazi wa vyombo vya habari na wageni waalikwa ndani ya chumba cha habari cha Vatican.
Kisha Francis akaelezea jinsi alivyofarijiwa na rafiki yake, Kardinali wa Brazil Claudio Hummes, wakati kura zikielekea upande wake na kuonekana 'hatari kidogo' kwamba angeweza kufikisha theluthi mbili muhimu kuweza kuchaguliwa.
Pale kilele kilipofikiwa, makofi yalilipuka kwenye kanisa dogo la Sistine lililotapakaa michoro ya sanamu ukutani.
"Yeye (Hummes) alinikumbatia. Akanibusu. Alisema usisahau kuhusu mafukara," Francis alikumbukia. "Na hivyo ndivyo moyo wangu ulipokuja na jina Francis wa Assisi," ambaye alijitolea maisha yake kwa ajili ya mafukara, kutangaza umisionari na kutunza uumbaji wa Mungu.
Alisema baadhi wameshangaa iwapo jina lake lilikuwa kumbukumbu ya watu wengine wa jina la Francis, akiwamo Mtakatifu Frances de Sales au pengine mwanzilishi mwenza wa amri ya papa ya Kijesuiti, Francis Xavier.
Lakini alisema alivutiwa mara moja baada ya uchaguzi huo pale alipofikiria kuhusu vita.
Mtakatifu Francis wa Assisi, papa huyo alisema, alikuwa "mtu wa mafukara. Mtu wa amani. Mtu ambaye alipenda na kujali uumbaji - na kwa hali hii hatuna uhusiano mkubwa kama huo na uumbaji. Mtu ambaye anayetupa roho yake ya amani, mtu fukara."
"Oh jinsi gani ningependa kanisa maskini na kanisa kwa ajili ya mafukara," Francis alisema, akivuta pumzi.
Mkutano huo katika Vatican umeanzisha wiki ya pilika kwa Baba Mtakatifu huyo ambayo inahusisha Ibada ya usimikaji itakayofanyika Jumanne ijayo.
Kati ya mazungumzo hayo, Vatican ilisema Jumamosi, kutakuwa na kikao na rais wa nyumbani kwa Francis Argentina kesho Jumatatu. Papa huyo amepingana vikali na Christina Fernandez dhidi ya msaada wake kwa kukarimu mambo kama ndoa za mashoga na ruhusa ya uzuiaji mimba.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item