JAMBAZI ANYWA SUMU MAHAKAMANI AKIJARIBU KUJIUA...

Gereza la Mahabusu Harare ambako Muza alikuwa akishikiliwa kusubiri hukumu yake.
Jambazi wa kutumia silaha amekimbizwa hospitali nchini Zimbabwe baada ya kwa namna ya ajabu kujaribu kujiua mahakamani, imeripotiwa.

Tendai Learnmore Muza, mwenye miaka 24, alikunywa sumu baada ya kuweka bayana kwamba anataka kufa pale alipotiwa hatiani katika matukio mawili ya ujambazi wa kutumia kisu Jumanne.
Mtuhumiwa huyo aliyekata tamaa alianguka katika sakafu ya kizimba kabla ya kukimbizwa hospitali kufuatia tukio hilo lisilo la kawaida kwenye mahakama ya hakimu mkazi katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Imeripotiwa kwamba Muza alitoa chupa hiyo ya sumu aliyotengeneza mwenyewe baada ya kudai alitiwa hatiani kimakosa kuhusiana na mashambulio mawili mabaya kwa kutumia visu.
Mbele ya hakimu Fadzai Mthombeni, aliweka wazi: "Mtukufu, ninataka kuungama.
"Ni bahati mbaya sana kwamba korti hii imenipata na hatia kwa makosa ambayo sikufanya.
"Mtu ambaye amefanya makosa haya anazurura mitaani bila wasiwasi, hivyo nimeamua kwamba suala langu litamalizwa mbinguni."
Imeripotiwa kwamba Muza, baba aliyeoa, kisha akatoa chupa ya plastiki ya ujazo wa mililita 500 iliyokuwa na mchanganyiko wa kemikali alizoziita 'dawa ya choo'.
Huku mahakama ikiwa kimya, aliongeza: "Mtukufu, ninataka ukamweleze mke wangu na watoto jinsi baba yao alivyokufa kwa kuwa najiua sasa hivi."
Polisi walikimbia kumwokoa mtuhumiwa huyo baada ya kuanguka sakafuni wakati wa matukio ya kushangaza Jumanne.
Muza alikimbizwa kwa matibabu ya dharura kwenye hospitali iliyoko ndani ya Gereza la Mahabusi mjini Harare, ambako hali yake ilielezwa juzi kwamba imeimarika.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa mwaka jana kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha baada ya yeye na wenzake kuwakamata maderena taksi wawili na kuwatishia kwa visu kisha kuwaibia fedha taslimu na simu zao za mikononi.
Muza alikuwa akishikiliwa mahabusu kusubiria hukumu yake, ambako alishitakiwa sambamba na mtu wa pili Tapera Maturiro, ambaye tayari anatumikia kifungo cha miezi 18 jela.
Maofisa magereza wameanzisha uchunguzi wa jinsi Muza alivyoweza kuingia na chupa ya kemikali aliyoitoa mahakamani.
Jaribio hilo la mtuhumiwa kutaka kujiua limekuja huku hakimu huyo akijianda kutoa hukumu kufuatia kutiwa kwake hatiani Jumanne.
Hakimu huyo alilazimishwa kuahirisha hukumu hiyo kutokana na vurumai hiyo.
Alieleza kwamba taratibu zinaahirishwa hadi tarehe nyingine itakayopangwa.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item