KAKA ADAIWA KUTUMIA JINA LA RAIS OBAMA KUJIPATIA FEDHA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/kaka-adaiwa-kutumia-jina-la-rais-obama.html
![]() |
| KUSHOTO: Malik Obama. JUU: Barack Obama akiwa pamoja na familia yake kabla ya kuukwaa Urais wa Marekani. CHINI: Barack Obama (kulia) wakati aliposimamia harusi ya kaka yake, Malik mwaka 1981. |
Malik Obama yamemfika shingoni maneno ya watu wanaomshutumu kwa kujaribu kujipatia fedha kwa kutumia jina maarufu la mdogo wake.
"Hili pia ni jina langu na haki yangu ya tangu kuzaliwa. Wasisahau kwamba nilizaliwa kabla yake," anasema.
Barack anaweza kuwa ameweka historia ya kuwa Rais mweusi wa kwanza wa Marekani, lakini si hivyo, Malik anasema, ndugu pekee wa familia hiyo anayetaka ukubwa.
Hiyo ilirindima ndani ya Malik, kutoka kwenye umri mdogo kabisa, kwamba alikuwa wa kipekee na hivyo alitarajia kuweka historia yake katika dunia hii.
"Baba yangu aliingiza hiyo taratibu kwetu sote," anasema. "Alikuwa akisema, "Bila kujali chochote, wewe ni bora zaidi, sababu nimetokea kwenye bidhaa bora zaidi. Siku zote hili likae akilini mwako."
"Na, kuwa mkweli, wakati mwingine kitu pekee kilichonifanya nisonge mbele kilikuwa ukweli kwamba mimi ni Obama; kwahiyo nilikuwa mtu fulani."
Wiki iliyopita, Malik mwenye miaka 54 alilazimishwa kuwa mpole katika imani yake hiyo baada ya kushindwa vibaya katika harakati zake za kusaka nguvu za kisiasa nchini Kenya.
Alisimama kama mgombea binafsi wa ugavana wa Jimbo la Siaya katika chaguzi za taifa.
Kama vile fedheha ya vipigo hadharani haikutosha kukabiliana nayo, Malik - anayeishi kwa kufuata sheria za Kiislamu - pia anakabiliwa na madai kwamba ni mpigaji mke na mzinifu aliyemnyanyasa Sheila Anyango, binti wa miaka 17, kwa maneno matamu na zawadi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 24, kisha kumfanya mke wake wa 12 wakati akiwa chini ya umri unaoruhusiwa kisheria.
Sheila aliwahi kusema: "Kuolewa naye [miaka mitatu iliyopita] imekuwa kosa kubwa katika maisha yangu. Ananipiga, lakini mara zote ni mwenye chuki na mpenda ugomvi." Binti huyo si wa kwanza kumtuhumu Malik kwa unyanyasaji.
Nimemkuta Malik akionesha majeraha yake kwenye makazi yake Barack H Obama Recreation And Rest Area pembezoni mwa Kogelo, kijiji chenye vumbi kisichofikika kwa urahisi ambacho ndiko makazi asilia ya familia hiyo.
Akiwa kavalia kawaida shati kubwa, suruali ya jeans na viatu vilivyong'arishwa kwa rangi nyekundu, Malik anaenda kwa kishindo ndani ya kitengo kikuu cha mgahawa. Ana urefu wa futi 6"4, mnene, anatembea akiwa kainama kidogo na kukamata mkono wangu katika salamu kama ile ya wakuu wa nchi ya kutingishana mikono.
Yeye na Barack wamechangia baba lakini hawafanani kwa muonekano. Wala yeye, kwa mujibu wa wote waliomsikia katika kampeni za uchaguzi, aliye msemaji mzuri.
Lakini ndugu hao wawili wanachangia mkataba, ulioghushiwa kutoka katika mkutano wa kwanza, ukubwani, miaka 27 iliyopita. Kila mmoja alikuwa msimamizi kwenye harusi ya mwenzake na kubakia kwenye mawasiliano ya kawaida - hasa kwa kuwa wote kwa sasa wanaishi mjini Washington DC.
Malik anamwelezea Michelle Obama kama 'mke Bora wa Rais' na anasema ametembelea Ikulu kwenye matukio kadhaa, kama ndugu wengine wa familia kubwa ya Obama.
"Ninaonana na mdogo wangu faragha angalau mara moja kwa mwaka, ninapokuwa nimekwenda kumtembelea Ikulu na kumsalimia. Ni kama kutembelea sanamu ya taifa inayofanya kazi, kama Smithsonian au Buckingham Palace.
Lakini mara zote amekuwa akipokea simu kama ninataka kuongea naye.
"Mara ya mwisho nilimwona Novemba 19 mwaka jana, muda mfupi baada ya uchaguzi wa Marekani. Nilikwenda Ikulu na kumpa pongezi zangu.
"Tuko karibu lakini hatuishi kwa kutegemeana kwa vipato. Sitakiwi kuwa katika kila sherehe kubwa. Sijamuona Michelle kwa kipindi kirefu mno.
Nilimwona yeye na watoto kwenye uzinduzi wa mwisho, lakini ilikuwa ni pilikapilika mno, hivyo hatukuwa na muda wa kuongea. Siwezi kusema kwamba nina mahusiano na wapwa zangu."
Malik ambaye kitaaluma ni mhasibu, anajitambulisha kama mshauri binafsi wa masuala ya fedha katika kampuni kadhaa za Marekani na kimataifa.
Analalamika kwamba anakashifiwa na kutoeleweka sababu yeye ni Muislamu na mtu mweusi. Sauti yake ni ya kina, yenye ladha ya Kimarekani - ameishi Washington tangu mwaka 1985 na kugawa muda wake kati ya mahali hapo na Kogelo.
"Kuwa na ndugu maarufu kumenifanya kuwa mlengwa wa chuki, ubaguzi wa rangi na mwenye kushika imani dhidi ya dini yangu," anasema. "Hivi karibuni nilimuuliza Barack ushauri gani angeweza kunipatia kuhusu kukabiliana na hizi fikra hasi.
Alicheka tu na kujibu, "Wewe ni mtu mzima. Wewe ni kaka yangu mkubwa, unaweza kukabiliana nayo. Usijali, ni miaka mingine minne tu."
Tangu wakati huo Malik anatarajia kukusanya fedha za kutosha kwa ajili ya kugombea urais wa Kenya, huku akitarajia kupambana katika miaka mitano.
Baadhi wanaweza kuuliza hamasa zake, lakini anasema Barack amekuwa akimhamasisha. "Mwaka 2011, nilipomweleza kuhusu mipango yangu, alisema niendelee nayo. Ushauri wake pekee ulikuwa ninatakiwa kuwa mkweli, mwaminifu - na kuwa imara."
Malik amebainisha jinsi alivyowahi kujaribu kutumia familia yake kubadili muundo wa siasa za kimataifa - kwa kumuomba mdogo wake kumwokoa Kanali Gaddafi wa Libya baada ya watu wake kumgeuka mwaka 2011.
"Nilikweda kumwona mdogo wangu na nilisema tazama, huyu ni mtu ninayemfahamu na inatisha kwa haya yanayoendelea. Hebu tuangalie kama tunaweza kuongea naye na kutafuta namna ya kumfikia tena. Hakushawishika na hilo.
"Hakutaka kufahamu, kitu ambacho kilikatisha tamaa mno. Lakini alinieleza kwamba walipeana mikono na Gaddafi wakati walipokutana kwenye mkutano mjini Roma."
Kisha akamkaripia Barack kwa kutofanya juhudi za kutosha kusaidia jamaa zake Wakenya.
"Najisikia fahari kwa mdogo wangu, lakini ningependa yeye afanye zaidi kidogo kwa ajili ya familia katika upande huu. Napenda kusema angetuma fedha kiasi. Ninatoa fedha ninapoombwa. Hiyo ni sababu ya kuwepo familia. Hatuko vizuri, ingawa watu wanadhani tuko hivyo."
Malik alikuwa na umri wa mwaka mmoja 1959 wakati baba yake, Barack Obama Senior, alipomwacha mkewe Kezia na kwenda masomoni katika Chuo Kikuu cha Hawaii. Dada wa Malik, Auma, mdogo kwa miaka miwili, anaonekana kuwa alikuwa mjamzito wakati baba yake aliporejea likizo nyumbani. Kezia, sasa ana miaka 72, baadaye alisoma Marekani na anaishi huko Bracknell, Berkshire.
Nchini Marekani, Barack Senior alikutana na kumuoa Ann Dunham, mwanaanthropolojia kutoka Kansas. Lakini muda mfupi baada ya kumzaa aliyekuja kuwa Rais wa Marekani, baba huyo akamtelekeza mama huyo na kurejea nchini Kenya.
Huko kulikuwa na wanawake wengine na watoto wengine, kabla ya kujiingiza kwenye tabia ya ulevi baada ya ajali ya gari iliyomwacha akiwa mlemavu. Rais huyo anasemekana kuwa alihangaika kuafikiana na kaka zake nane na madada kutoka kwa mama wanne tofauti.
Malik anakumbushia: "Baba yangu alirejea mwaka 1964 na tuliishi hapa Kogelo, kabla ya kuhamia Nairobi. Alikuwa meneja mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Utalii Kenya, ambayo ilikuwa kazi nzuri mno. Tulikuwa na kila kitu bora - gari nzuri, nyumba ya kupendeza, na watumishi.
"Lakini tulipoteza vyote baada ya ajali mwaka 1971 sababu hakuweza tena kufanya kazi. Nilikuwa nasoma katika moja ya shule bora kabisa binafsi, lakini ghafla nikalazimika kuwa natembea maili kumi kufika hapo.
"Kulifikia wakati ambapo hatukuwa hata na pesa za chakula. Nililazimika kuomba chakula kutoka kwa wanafamilia wengine. Ilikuwa ngumu kushuhudia kuangamia kwa baba yangu. Alifariki akiwa na miaka 46, bila kutuachia chochote."
Baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi akiwa na shahada ya Uhasibu, Malik alifanya kazi mjini Nairobi hadi mwaka 1985, pale alipohamia nchini Marekani.
"Barack alifanya mawasiliano mara baada ya kuanza kuishi mjini Washington na kusafiri kutoka Chicago, kuja kuonana nami," anasema. "Nilifahamu kuhusu yeye tangu mwanzo, sababu baba yangu alikuwa akimzungumzia mno."
Malik, ambaye anamiliki duka dogo la vifaa vya umeme mwendo wa nusu saa nje ya Washington, anasema hakuna kosa lolote kutumia jina lake kama shinikizo la mabadiliko - lakini anaongeza kwamba familia ya mdogo wake haihusiki.
"Wamejitoa," alisema. "Hawahusiki katika ninachofanya. Anafanya mambo yake, yeye ni Rais wa Marekani. Mimi ni Malik Obama, ninayefanya kitu hiki.
Anadai kuwa amekusanya karibu Dola za Marekani 100,000 kwa ajili ya mfuko wake, taasisi aliyoianzisha mwaka 2008 'kutenda mema kwa ajili ya Kogelo'.
Akihamia katika shutumu kuhusu maisha yake ya nyumbani, alikanusha vikali madai hayo dhidi yake.
"Siwapigi wake zangu, kama ambavyo imekuwa ikidaiwa. Mara kwa mara nimekuwa nikikanusha madai hayo yanayokuja kutoka kwa mke wangu," anasema.
"Sheila alirudi nyumbani kwa mama yake siku iliyofuata baada ya kuwa amekosana na mke mwenzake kwenye eneo la familia yetu. Sitaki kuingia kwa undani, lakini ilikuwa ni kati ya wanawake wawili, haihusiani na mimi.
"Alikuja na mimi kwenye kituo cha kupigia kura Jumatatu iliyopita na kuniambia bado ananipenda. Nina hakika atakuwa nyumbani kwangu wakati atakuwa tayari."
Malik anasisitiza ni mtu mpenda usawa. "Kumekuwa na wake 12 tangu ndoa yangu ya kwanza mwaka 1981, wakati Barack alipokuwa msimamizi wangu. Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kwa wote, sambamba na watoto." Hakutaka, hatahivyo, kusema ni wangapi alionao.
Anatarajia kwa kuwania ugavana kutampaisha kimataifa.
"Usishangae kama, katika kipindi cha miaka mitano, kuna rais mwingine mwenye jina la Obama."