KOCHA AKABILIWA NA KIFUNGO KWA KUDHALILISHA WASICHANA KWA MIAKA 40...

Mmoja wa makocha mashuhuri wa mazoezi ya viungo nchini Uingereza anakabiliwa na kifungo jela kwa kuwadhalilisha wasichana wadogo sita kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Bob Bellew amechapisha vitabu kuhusiana na mchezo huo, vinavyotumika kufundishia mashuleni kote mjini London na aliwahi kuwa Kocha Bora wa Mwaka.
Pia alitumikia katika kamati za mipango za Olimpiki zilizofanyika London na alikuwa Kocha Mkuu wa timu za Shule za Hamlets wa Sarakasi na Maonesho ya Muziki.
Kocha huyo mwenye miaka 66 aliweza hata kutunukiwa tuzo ya 'The Order of the Smile,' inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa iliyolenga 'watu wazima wenye mapenzi, kujali na kusaidia watoto'.
Lakini kwa karne kadhaa kocha huyo anayeheshimika aliwawinda wasichana aliokuwa akiwafundisha, Mahakama ya Snaresbrook ilielezwa.
Alikiri kuwapapasa wasichana hao, wenye umri wa kuanzia miaka 13 hadi 15, kati ya Septemba 18, 1970, na Desemba 14, 2010.
Baadhi ya udhalilishaji ulifanyika wakati wa safari nje ya nchi na wakati wa madarasa ya sarakasi.
Bellew alikiri mashitaka manane kati ya 17 dhidi yake, yanayohusisha waathirika sita na kuanzia nyuma mwaka 1970 kwenye kesi katika Mahakama ya Snaresbrook.
Aliungama kuwaguza na kupenyeza mguu wake chini ya sehemu za siri za msichana, kusugua mapaja yao na kuwachokoa na kuwashika makalio.
Bellew, anayetokea New Cross, kusini mwa London alikiri mashitaka saba ya kwenda kinyume na maadili na moja la kugusa kwa lengo la kimapenzi.
Mashitaka aliyokana yataachwa yabaki kwenye kabrasha, na atahukumiwa kwa mashitaka manane aliyokiri ifikapo Aprili 11.
Aliachiwa kwa dhamana kwa sharti kwamba hatakiwi kuonana na muathirika yeyote kati yao.
Bellew alichapisha vitabu kadhaa vya ukocha wa mazoezi ya viungo kikiwamo alichokipa jina "Gymnastics: A Flying Start in 1993".

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item