LOWASSA AONYA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/lowassa-aonya-wabunge-wa-afrika.html
Edward Lowassa. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa amewatahadharisha wabunge wa Afrika Mashariki kuwa Watanzania hawatawaelewa iwapo vikao vya Bunge vitaendelea kufanyika nje ya Mji wa Arusha ambako ni makao makuu ya jumuiya hiyo.
Lowassa ambaye Kamati yake jana ilikuwa inapokea mapato na matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alihoji sababu ya Bunge hilo kuzunguka katika nchi wanachama wakati tayari makao makuu ya jumuiya hiyo yako tayari katika Mji wa Arusha.
Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhanji katika kujibu swali hilo, alisema sababu inayofanya wazunguke kila nchi kufanyia vikao vyao ni kutokana na mapendekezo ya Spika pamoja wabunge wa Bunge hilo.
"Kwa mwaka huu ni ngumu kurekebisha kwa vile tayari ratiba ya vikao imeshapangwa na vikao vitatu vimeshafanyika Arusha, Nairobi na Bujumbura, vikao vijavyo vitafanyika katika miji ya Kigali na Kampala," alisema Bhanji.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta aliiambia kamati hiyo Wizara yake ingependa kuona asilimia 50 ya vikao hivyo inafanyika makao makuu ya jumuiya hiyo ambayo yako mjini Arusha.
"Hakuna haja ya kuwa na jengo la namna ile makao makuu halafu vikao havifanyiki," alisema Sitta na kubainisha kuwa Tanzania imekataa mapendekezo ya baadhi ya nchi wanachama ambao walitaka vikao vya Mahakama ya Afrika Mashariki viwe vinafanyika kwa zamu katika nchi wanachama.
Katika kuchangia hoja hiyo, Makongoro Nyerere alisema mkataba wa Afrika Mashariki ndio unaelekeza vikao hivyo kufanyika sehemu yoyote na unaelekeza kuwa ni lazima ufanyike walau mara moja kwa mwaka.
"Sisi wabunge hatuna mamlaka ya kubadilisha, wanaoweza kubadilisha ni Baraza la Mawaziri ambao watapendekeza kwa wakuu wa nchi wanachama," alisema Makongoro kauli ambayo ilimshangaza Lowasa na akahoji "Kweli nyie hamna mamlaka ya kubadilisha suala hili?”
Swali hilo lilimlazimu Waziri Sitta kuusoma mkataba huo unaoelekeza hivyo; lakini akawashangaa wabunge hao wa Tanzania kuwa watakuwa wamekwepa wajibu wao kama hawatakuwa na msimamo ili mikutano ya Bunge lao ifanyike makao makuu ya jumuiya hiyo na sio vinginevyo.
Abdallah Mwinyi ambaye amedumu katika Bunge hilo kwa vipindi viwili, alisema uamuzi wa kufanya vikao hivyo katika nchi wanachama unafanywa na Spika kwa kushirikiana na Kamati ya Uongozi ambayo Tanzania ina wajumbe wawili.
"Katika ile Kamati kila mtu anatamani vikao vya Bunge hilo viende nchini mwake, hivyo ni ngumu kwa wajumbe wawili wa Tanzania kuwashinda maana maamuzi ya vikao vyetu yanaegemea kwenye wingi," alisema Mwinyi na kuongeza kuwa Kamati hiyo ya Uongozi ina wajumbe 11.