HATIMAYE MWIZI MZOEFU WA SIMU ZA MKONONI ATUPWA JELA MIEZI 20...

KUSHOTO: Calin-Lonel Rostas. KULIA: Rostas (aliyezungushiwa duara) akijiandaa kufanya wizi wake ndani ya mkahawa.
Kibaka wa Romania ambaye aliwalaghai wateja wa mkahawa kwa kutumia vipande vya karatasi zilizopangwa kama 'ngao' huku akiwaibia simu zao, ametupwa jela jana.

Calin-Lonel Rostas mwenye umri wa miaka 27, alinyakua kwenye mikahawa na popote alipoona simu ya mkononi imeachwa juu ya meza kwa kuweka kipande cha karatasi ukubwa wa A4 juu yake.
Kisha baadaye anawazuga wamiliki wa simu kwa kuongea nao kwa vitendo kuhusu hali ya hewa kabla ya kutumia vidole vyake vyepesi kuzishushia simu hizo ndani ya mfuko wake huku akichukua kipande chake cha karatasi.
Waathirika hubaini tu kwamba simu zao zimeibwa mara baada ya Rostas kuondoka mkahawani hapo kufuatia wizi wake unaotumia chini ya sekunde tano.
Rostas amefanikiwa kutokomea na simu takribani 15 zenye thamani ya Pauni za Uingereza 6,000 (zaidi ya Sh. milioni 15,000 za Kitanzania), lakini alikamatwa baada ya polisi kupitia kwa masaa picha za kamera ya CCTV katika mikahawa mjini Manchester ukiwamo Starbucks, Costa Coffee, Cafe Nero na mikahawa miwili ya chuo kikuu cha jiji hilo.
Wakati alipokamatwa ilidaiwa ndio kwanza alikuwa ameachiwa kutoka jela kwa makosa kama hayo.
Jana mzaliwa wa Romania, Rostas, kwa sasa anaishi huko Crumpsall, Manchester amehukumiwa kifungo cha miezi 20 jela.
Alipatikana na hatia kwa matukio 15 ya wizi na majaribio matano ya wizi, ikiwamo simu nne za mkononi na iPad moja na alisemekana kuwa na historia ya kufanya matukio 13 ya utapeli tangu mwaka 2002.
Mahakama ya Manchester ilielezwa kwamba Rostas alilenga mikahawa na migahawa iliyoko katikati ya jiji la Manchester na kusini mwa Manchester kati ya Desemba mwaka jana na Februari.
Hatimaye alikamatwa baada ya kujaribu kuwaibia wanafunzi waliokuwa wakinywa kahawa nje ya mgahawa wa McDonalds kwenye Barabara ya Oxford. Katika taarifa iliyokabidhiwa kwa polisi, waathirika hao wanasemekana walibaki wakiwa na 'hofu na tahayari."
Mwanamke mmoja amekuwa mwenye mashaka, wengine wakijilaumu wenyewe na mmoja wa waathirika amekatisha mtihani wa chuo kikuu kufuatia wizi huo.
Baadhi ya vipande vya karatasi ambavyo Rostas alitumia vilikuwa na miandiko yao, na pia alitumia vishina na kujifanya kama ombaomba akitaka pesa. Rostas alisema aliuza simu hizo kulipia madeni ya kamari. Simu hizo hazikuwahi kupatikana.
Polisi wamebainisha taarifa za wizi unaofanana na huo unaohusisha mbinu kama hizo eneo lote na Greater Manchester, huku tukio moja linalofanana na wizi kama huo likiwa limeripotiwa hivi karibuni kwenye baa mjini Prestwich, karibu na Bury.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item