MAKARDINALI KUANZA KUCHAGUA PAPA MPYA JUMANNE IJAYO...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/makardinali-kuanza-kuchagua-papa-mpya.html
![]() |
| Wafanyakazi wakiandaa vifaa kwa ajili ya mkutano huo wa faragha Jumanne ijayo. |
Jumanne mchana makardinali wataanza mkutano wao wa faragha kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki mjini Roma.
Msemaji wa Vatican alitangaza jana kwamba makardinali watafanya mkutano wa faragha katika Kanisa dogo la Sistine baada ya misa ya asubuhi katika St. Peter's Basilica.
Mbali na kula na kulala, hawataruhusiwa kuondoka kwenye mkutano hadi watakapokuwa wamechagua atakayemrithi Papa Benedict XVI, ambaye alitangaza uamuzi wake wa kustaafu ghafla Februari 10, mwaka huu.
Ijumaa asubuhi, makardinali walipokea barua za maelezo kutoka kwa makardinali wawili wapigakura ambao wanaruhusiwa kupiga kura kuchagua papa ajaye lakini hawatahudhuria mkutano huo.
Mmoja kati yao alikuwa Keith O'Brien wa Scotland, ambaye alielezea sababu binafsi.
Wote ambao wanahusika katika upigaji kura sasa wameshawasili mjini Roma, tayari kwa kuanza mkutano huo Jumanne ijayo.
Huku vikao kwa ajili ya mkutano huo wa faragha vikiwa vimechelewa mjini Roma wiki hii, Papa wa zamani Benedict XVI, mwenye umri wa miaka 85, alionekana katika picha akitembea kwa msaada wa fimbo maalumu kwenye bustani ya makazi yake iliyoko Castel Gandolfo pembezoni mwa mji wa Roma ambako atakuwa akiishi kwa muda hadi atakapopatiwa makazi mapya - jengo la kitawa linalokarabatiwa kwenye viwanja vya Vatican limekamilika.
Kiongozi wa zamani wa Kanisa Katoliki ataishi hapo Castel Gandolfo kwa wiki kadhaa, akilala kwenye kitanda chenye upana wa sentimeta 75 tu na bila mwavuli.
Kisha baadaye atahamia kwenye makazi yaliyoandaliwa maalumu kwenye jumba la kitawa katika Vatican.
Baba Mtakatifu mstaafu ameripotiwa kuchukua vitabu kadhaa vya theolojia pamoja na muziki kwa ajili ya kusikiliza.
Pia alikuwa akitarajia kujiliwaza kwa kupiga piano - moja ya vitu anavyopendelea katika kujiliwaza - nyakati za jioni.
Zaidi ya makardinali 150 walihudhuria siku ya tatu ya vikao vya awali kuandaa sifa za Papa ajaye kufuatia uamuzi wa kushitua wa Papa Benedict mwezi uliopita.
Vikao hivyo vya awali vinafanyika huku balaa linalohusisha udhalilishaji wa kijinsia wa watoto unaofanywa na watawa na tabia zisizokubalika miongoni mwa mapadri wakongwe vikiendelea kulitafuna kanisa hilo na mara kadhaa vimekuwa vikitawala vichwa vya habari kwenye vyombo mbalimbali.
Chini ya sheria ya Kanisa makardinali hadi Machi 20 kuwa wameanza mkutano wa faragha kuchagua Papa mpya kuongoza wafuasi bilioni 1.2 wa Kanisa hilo.
Wakati wachunguzi wengi wamebashiri mkutano huo wa siri utaanza mapema Jumapili hii au Jumatatu, kumekuwa na ongezeko la viashiria kwamba makardinali wanataka muda zaidi kuchanganua yupi kati yao anaweza kuwa bora zaidi kuongoza Kanisa linaloshambuliwa na migogoro.
Wafanyakazi wameshaanza kuandaa ndani ya Kanisa dogo la Sistine, kujenga upya, sakafu iliyotelekezwa kulinda vigae vya karne nyingi.
Wafanyakazi walionekana kwenye picha wakifunga stovu ndani ya kanisa ambako masanduku ya kura yanachomwa pale kura zitakapokuwa zimepigwa.
Stovu hizo zimening'inizwa katika chemli kwenye dari na mawimbi ya moshi mweupe kutoka humo wakati Papa mpya atakapokuwa amechaguliwa.

| Hivi ndivyo mchakato wa kupata Papa mpya unavyokuwa. |