MAZIKO YA BILIONEA WA ARUSHA SASA UTATA MTUPU...

Marehemu Nyaga Mawalla.
Maziko ya mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Nyaga Mawalla, yameingia katika utata baada ya familia kushindwa kuamua wapi mahali pa kuzikwa.
Mawalla, bilionea kijana ambaye hajafikisha miaka 40, alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Nairobi alikokuwa amelazwa wiki mbili zilizopita, baada ya kwenda kupata matibabu ya maradhi ya ugonjwa wa moyo yaliyokuwa yakimsumbua.
Habari kutoka ndani ya familia zilisema kuwa utata ulizuka juu ya wapi marehemu utazikwa, baada ya kujitokeza madai kwamba Mawalla aliwahi kuacha wosia kuwa atakapokufa, azikwe Momela wilayani Arumeru, kwenye shamba lake la ekari tatu.
Vyanzo vya habari kutoka katika familia iliyoanza vikao tangu juzi, vilisema kuwa mama mzazi wa marehemu ambaye jina lake halikupatikana mara moja, amekuwa akisisitiza kuwa mwanawe kipenzi, azikwe nyumbani kwao Marangu Moshi na si mahali pengine popote.
Kutokana na utata huo, taarifa zinasema vikao vya familia viliazimia kumsubiri mdogo wa marehemu, Wilfred Mawalla ambaye yuko jijini Nairobi.
Wilfred yuko nchini Kenya, akishughulikia uchunguzi wa madaktari na kusafirishwa kwa mwili wa marehemu na ndiye anayetajwa kusubiriwa kumaliza mzozo huo.
"Vikao vimeahirishwa juu ya utata huo, sasa tunamsubiri mdogo wa marehemu ili aje azungumze na mama yake, watupe jibu wapi marehemu atazikwa. Hapa tulipo
sisi hatuna uamuzi kabisa,’’ alisema mtoa habari.
Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete leo anatarajia kuongoza maelfu ya wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha katika maziko ya mfanyabiashara Hendri Nyiti, yatakayofanyika Tengeru wilayani Arumeru.
Nyiti alifariki dunia wiki iliyopita mjini Mahenge, wilayani Ulanga, baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa malaria.
Baada ya kifo chake, wafanyabiashara wenzake wa madini walikodi ndege maalumu hadi jijini Arusha katika uwanja mdogo wa Arusha, na kuupeleka mwili kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item