MWANDISHI WA NYIMBO KALI ZA KUNDI LA JACKSON 5, DIANA ROSS AFARIKI DUNIA...

KUSHOTO: Kundi la Jackson 5 enzi hizo. KULIA: Deke Richards.

Mwandishi na Prodyuza mkongwe wa nyimbo wa Motown, Deke Richards amefariki dunia kwa maradhi ya saratani kwenye hospitali ya wagonjwa mahututi katika jimbo la Washington. Alikuwa na umri wa miaka 68.
Richards, ambaye nina lake halisi ni Dennis Lussier, alifariki Jumapili kwenye nyumba ya wagonjwa ya Whatcom, msemaji wa Peace Health St Joseph Medical Center, Amy Cloud alithibitisha jana.
Richards amekuwa akipambana na saratani, kwa mujibu wa taarifa kutoka Universal Music.
Alikuwa kiongozi wa timu ya uandishi, mpangilio na utengenezaji muziki ya Motown inayofahamika kama The Corporation, ambayo ilikuwa chini ya waasisi wa Motown Records Berry Gordy, Alphonzo Mizell na Freddie Perren.
Richards alijikita kikamilifu katika kuandika na kutengeneza nyimbo nyingi zilizotamba za Jackson 5, kwa mujibu wa taarifa kutoka Universal Music.
Nyimbo hizo ni pamoja na vibao vikali vitatu vya mwanzo vya Jackson 5 - "I Want You Back," "ABC," na "The Love You Save."
Akizungumza baada ya kifo cha Michael Jackson mwaka 2009, Richards alisema kwamba Mfalme huyo wa Pop alikuwa na 'akili za kuzaliwa.'
Pia alishiriki kuandika nyimbo kama "Love Child" ya Diana Ross & The Supremes, vilevile wimbo binafsi wa Diana Ross wa "I'm Still Waiting."
Wasanii wengine ambao Richards alitengeneza au kuandika nyimbo zao ni pamoja na Bobby Darin, The Four Tops na Martha Reeves & the Vandellas.
Richards ameacha mke, Joan Lussier, kaka na wapwa zake wawili.
Mipango ya kufanya sherehe ya faragha ya familia kusherehekea maisha yake inaendelea.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item