MTOTO WA MWANAMIELEKA MKONGWE AFARIKI DUNIA...

KUSHOTO: Reid Fliehr. KULIA: Mwanamieleka mkongwe, Ric Flair.
Mtoto wa kiume mwenye miaka 25 wa mwanamieleka mkongwe, Ric Flair amefariki dunia.

Wakala wa Flair ameeleza: "Tunasikitika kuthibitisha kwamba mtoto wa Ric, Reid Fliehr, amefariki dunia leo (jana) Machi 29, 2013 huko Charlotte, NC."
Wakala huyo ameendelea: "Uchunguzi kuhusiana na sababu za kifo chake unaendelea."
Reid alikuwa mwanamieleka wa kujitegemea ambaye alikuwa akicheza mchezo huo nchini Japan kwa kipindi cha miezi michache iliyopita. Pia aliwahi kucheza kwa muda mfupi katika WCW kama mtoto.
Reid alihusishwa na matumizi ya dawa za kulevya aina ya heroin kipindi cha nyuma, na aliwahi kukamatwa mwaka 2009 kwa kupatikana na dawa hizo.
Wakala wa Ric anasema: "Hakuna neno linaloweza kutosheleza machungu ambayo Ric na familia yake wanapitia na wameomba faragha wakati huu wa maombolezo."
Ilielezwa kwamba mamlaka husika zilipokea simu kutoka kwa mtu aliyesema alimwona mtu aliyekuwa hajiwezi kwenye chumba cha hoteli. Wapelelezi walifika eneo la tukio na kumkuta Reid, ambaye alikuwa tayari amekwishakufa.
Imeelezwa hakuna dalili zozote za kwamba alikuwa ameuawa.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item