ATAMBA NA KICHWA CHA MWENZAKE MITAANI MWANZA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/atamba-na-kichwa-cha-mwenzake-mitaani.html
Kamanda Ernest Mangu. |
Mkazi mmoja wa eneo la Bugarika jijini Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira baada ya kufanya mauaji kwa mwenzake kwa kumtenganisha kichwa, kisha kuanza kutamba nacho mtaani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa 7 na saa 8 mchana maeneo ya Bugarika. Watu hao wawili waliokufa ni Bahati Vicent na Malimi Mathias ambao inadaiwa wakati wa uhai walikuwa karibu sana.
Akifafanua, Kamanda Mangu alisema watu hao wawili walikuwa wanakunywa pombe katika kilabu ya pombe za kienyeji wakati walipoanza kugombana wakidaiana fedha.
Alisema watu hao ambapo mmoja ni mmliki wa kilabu hiyo walianza kudaiana fedha na baada ya kuzozana kwa muda, Malimi alimkaba Bahati na kisha kumchinja na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.
Kamanda huyo wa polisi alisema baada ya kufanya mauaji hayo alianza kutembea mtaani na kichwa cha marehemu Bahati na kuwaonesha watu ambao baada ya kuona unyama huo walipigiana yowe na kujitokeza kwa wingi na kuanza kumshambulia Malimi hadi kufa.
Alisema Polisi walipofika katika eneo hilo walikuta miili ya wawili hao na kuipeleka Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Alisema marehemu wanadaiwa kuwa marafiki wa karibu na kwamba walikuwa mafundi wa ujenzi.
Akizungumzia Sikukuu ya Pasaka Mangu alisema Polisi wamejipanga vyema kukabiliana na tishio la usalama kwenye Makanisa na kutaka wananchi kusherehekea kwa amani.