MWALIMU ADAIWA KUSHAWISHI WANAFUNZI WA KIKE WAMTUMIE PICHA ZAO ZA UTUPU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/mwalimu-adaiwa-kushawishi-wanafunzi-wa.html
Mwalimu wa zamani wa sekondari ya juu anatuhumiwa kuwashawishi wanafunzi wa kike wenye umri mdogo kumtumia picha zao wakiwa watupu na kwa kuwa na mahusiano na msichana mwnye miaka 17.
Jon Erik Lilly kutoka Cedar Lake, Indiana alikamatwa juzi Jumatano kwa mashitaka kwa kumiliki michoro inayochochea kujiingiza katika vitendo vya ngono.
Polisi wanasema mwalimu huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 27 wa Morton High School alikuwa akiwasiliana na wasichana wanne walio chini ya umri kwa kutumiana meseji za ngono wakati akiwa anafundisha kwenye shule hiyo iliyoko Hammond.
Katika kompyuta yake ya nyumbani wachunguzi wanadaiwa pia kukuta picha za utupu za wasichana tofauti wasiopungua 10.
Takribani wanne wamekadiriwa kuwa na umri mdogo wakati picha hizo zilipokuwa zikipigwa.
Uchunguzi dhidi ya Jon ulianza pale mama wa mwanafunzi huyo mwenye miaka 17 kuitaarifu polisi anahisi binti yake kwamba ana mahusiano na mwalimu wake huyo.
Madai yote yaliwekewa uzito na wanafunzi wengine shuleni hapo, kwa mujibu wa taarifa, ambao wamesema kuwa wao pia walifahamu kuhusu mahusiano yao.
Kumbukumbu za mahakama zilizofunguliwa Jumatano zinasema mnamo Novemba ofisa wa shule alikamatwa akiwa ameketi na mwanafunzi wa kike katika ya miguu yake akimshawishi mtawala huyo kumwandika.
Msichana huyo aliyehusishwa kwanza alikanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Jon lakini baadaye alikiri wawili hao kufanya mapenzi kwa kwa miezi minne iliyopita au zaidi.
Jon amekanusha kuhusiana kimapenzi na binti huyo huku akisisitiza alikuwa akisubiria hadi atakapotimiza umri wa miaka 18, kwa mujibu wa mamlaka.
Hakuweza kupatikana kwa maoni sababu namba yake ya simu haikuwa imeorodheshwa.