MWANAMKE AOLEWA NA NDUGU WATANO, HAJUI YUPI BABA WA MTOTO...

Rajo Verma na mwanae akiwa amesimama mbele ya waume zake ndugu watano.
Mwanamke wa Kihindi amezungumzia kuhusu kuolewa na waume watano, wote wakiwa ni ndugu.

Rajo Verma, 21, anaishi katika chumba kimoja na ndugu hao na wanalala kwenye mablanketi sakafuni.
Mama huyo wa mtoto mmoja, ambaye analala kila usiku na ndugu tofauti, hafahamu kati ya waume zake hao watano nani hasa ni baba wa mtoto wake mwenye umri wa miezi 18.
Utaratibu huo unaweza kuonekana wa kipekee, lakini ni utamaduni katika kijiji hicho kidogo karibu na Dehradun, Kaskazini mwa India, kwa wanawake kuoa pia ndugu za mume wa kwanza.
Amelieleza gazeti la The Sun: "Awali waliona kidogo kinyume. Lakini mimi sifanyi upendeleo kwa yeyote kati yao."
Rajo na mume wa kwanza Guddu walioana katika ndoa iliyopangwa ya Kihindu miaka minne iliyopita.
Tangu wakati huo amemuoa Baiju, 32, Sant Ram, 28, Gopal, 26, na Dinesh, 19 - wa hivi karibuni katika mstari wa waume - ambaye alimuoa mara tu alipotimiza umri wa miaka 18.
"Sote tunafanya nae mapenzi lakini hatuna wivu," mume wa kwanza Guddu - ambaye anabaki kuwa mume rasmi - alisema. "Sisi ni familia moja kubwa yenye furaha."
Utamaduni wa kale wa Kihindu wa kuoa waume wengi ulikuwa ukitumika sehemu kubwa ya India, lakini kwa sasa unafanyika kwa watu wachache tu.
Inashuhudiwa mwanamke akioa zaidi ya mume mmoja, hasa katika maeneo yote ambayo yametawaliwa na watoto wa kiume.
Katika ndoa za wanaume wengi wa kindugu, mwanamke inatarajiwa kuoa kila ndugu wa damu wa mume wake.
Zoezi hilo linaaminika kuwa na lengo la kuhifadhi ardhi kwa ajili ya kilimo.
Hii imekuwa maarufu sana kutokea kwenye maeneo ya milima ya Himalaya kaskazini mwa nchi hiyo, na hata kwenye taifa lenye milima la Tibet.
Rajo alisema yeye alijua yeye alikuwa anatarajiwa kukubali waume zake wote, kama mama yake alivyooa ndugu watatu.
Alisema wanalala pamoja kwa zamu, lakini hawana vitanda, ila tu mablanketi mengi juu ya sakafu."
Aliongeza: "Mimi hupata umakini zaidi na upendo kuliko wake wengi."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item