RAIS KIKWETE AKUBALI KUWA MLEZI WA 'WABWIA UNGA'...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/rais-kikwete-akubali-kuwa-mlezi-wa-unga.html
Rais Jakaya Kikwete. |
Rais Jakaya Kikwete, juzi usiku alikuwa na mazungumzo na waathirika wa dawa za kulevya wa Wilaya ya Kinondoni wanaotibiwa Hospitali ya Mwananyamala.
Baada ya kusomewa risala, waathirika hao waliomweleza namna walivyoathirika na dawa hizo na mabadiliko waliyonayo baada ya tiba.
Mmoja wa waathirika hao ambaye ni mkazi wa Mbagala, Shaban Selemani (32), alimwomba Rais amnunulie bajaj, afanyie kazi na kutembelea kwenye mizunguko yake, kwa maelezo kuwa amejitambua na kuona umuhimu wa kujitafutia kipato kwa njia halali.
Kwa sababu alikuwa katika kiti cha matairi cha wagonjwa, Rais alitaka kujua kilichomsibu mpaka kupata ulemavu huo.
Selemani alijibu, “ndio hivyo tena” na kufafanua kwamba ni matokeo ya ajali iliyotokana na harakati zake za kutafuta, wakati alipokuwa ‘akibwia unga’.
Katibu wa Chama cha Waathirika Wanaotibiwa (MAT), Nabila Khan, alisema alikabiliwa na mazingira magumu kiasi cha kujiuza mwili ili apate fedha za kununua dawa hizo za kulevya.
“Mheshimiwa Rais, tumeuza miili ili tupate fedha kidogo tu ya kununua dawa za kulevya, unavyotuona hapa wote tumefanya uporaji na wizi kuanzia nyumbani tunapoishi hadi mitaani.
“Lakini yote hayo ni ili tusikose kiasi kidogo cha kununulia dawa, sasa tunakuahidi kutoyarudia hayo, na jamii hainabudi kutuamini kwa sababu matibabu yametuondolea ile hamu iliyokuwa ikitusukuma kufanya hayo,” alisema Khan.
Katika risala ya MAT, iliyosomwa na Anord Kommu ambaye ni Makamu Mwenyekiti, alimwambia Rais kuwa wanajua jinsi anavyowahangaikia ili wapone, hivyo asijali kwa sababu hawatamwangusha kwa kuyarejea matapishi yao.
“Lakini, ili tutimize ahadi hii, Mheshimiwa Rais, tunaomba ukubali kuwa mlezi wetu na utusaidie kurasimisha kikundi chetu ili kiwe asasi ya kijamii yenye usajili unaotambulika kisheria...“Kwa kufanya hivyo, tutakuwa na uhuru wa kutoa ushauri kwa wenzetu wanaoendelea kuathiriwa na dawa za kulevya,” alisema Kommu.
Rais Kikwete alikubali kuwa mlezi wao. “Mkuu wa Mkoa, Meck Sadick, atanisaidia lakini ni lazima mkutano wa kwanza nanyi niufungue mwenyewe, ili nijue hasa ni nini tatizo na ni namna gani tunaweza kushirikiana kulitatua,” alisema.
Wakati huo huo wanakikundi hao walimshangilia Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na kung’ang’ania kupiga naye picha kwa kutumia simu zao, huku wakimwambia kuwa wamemuona.