WANAOMTETEA LWAKATARE WAANDAA HATI YA DHARURA...

Tundu Lissu.
Mawakili wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake, wanatarajia kupeleka  ombi kwa hati ya dharura Mahakama Kuu, ili iingilie kati   haki itendeke.

Juzi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), alipeleka hati ya kuwafutia mashtaka ya ugaidi Lwakatare na mwenzake, lakini walikamatwa tena na kusomewa upya mashitaka manne likiwemo la ugaidi.
Akizungumza jana Dar es Salaam katika ofisi za Chadema, mmoja wa mawakili hao, Tundu Lissu, alisema hati hiyo ya dharura inaiomba Mahakama Kuu kuangalia mafaili yote ya kesi ya Lwakatare kabla ya kuachiwa, na baada ya kukamatwa tena kama kweli yanatenda haki.
“Leo (jana) hati ya dharura itapelekwa ili Mahakama Kuu ichunguze ione kama haki imetendeka kwa mujibu wa Katiba,” alisema Lissu.
Kadhalika alisema kupitia hati hiyo, wataiomba Mahakama kama itakubali, ifute hati iliyofuta ile kesi ya mwanzo ya Lwakatare, pamoja na amri ya kumaliza kesi iliyokuwa mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru.
Alisema baada ya hilo, pia wanaiomba Mahakama hiyo ielekeze Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itoe uamuzi kama ilivyokuwa awali kabla ya kesi kufutwa.
Lissu alisema chini ya hati hiyo ya dharura, wanaiomba Mahakama Kuu, itamke kuwa walichokifanya mawakili wa Serikali,  ni matumizi mabaya ya kuingilia uhuru wa Mahakama kutenda haki katika kesi hiyo.
Lissu alisema hakuna mashitaka mapya aliyokamatwa nayo Lwakatare, zaidi ya yale yale ya zamani, labda ni kubadilika kwa namba ya kesi kutoka 37 ya 2013  na kuwa 6 ya 2013, na  hakimu mwingine ambaye ni Hakimu Mkazi Aloyce Katemana.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item