UHURU AREJEA IKULU ALIKOISHI NA BABA YAKE TAKRIBANI MIAKA 15...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/uhuru-arejea-ikulu-alikoishi-na-baba.html
![]() |
| Uhuru Kenyatta siku alipokuwa akipiga kura. |
Yametimia nchini Kenya kwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa muasisi wa Taifa hilo kushinda uchaguzi wa urais kwa tofauti ndogo ya asilimia 50.07 ambao unatosha kuzuia marudio ya uchaguzi huo.
Kutokana na matangazo ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) jana katika jengo la Bomas of Kenya, jijini Nairobi na kushuhudiwa na mamilioni ya watu duniani, sasa Kenya inakuwa nchi ya pili ya Kiafrika baada ya Sudan, kuwa na kiongozi aliye madarakani huku akikabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa IEBC, Issack Hassan, alisema mshindi alipata jumla ya kura 6, 173,433 kati ya 12, 330, 038 zilizopigwa. Baada ya kutangaza matokeo hayo, Kenyatta aliingia akifuatana na Makamu wa Rais Mteule William Ruto ambapo Rais Mteule alikabidhiwa cheti maalumu cha kumwidhinisha kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Tangu alfajiri jana wafuasi wa Kenyatta waliolemewa na furaha, waliingia mitaani hasa katika maeneo ambayo ni ngome yake wakifyatua fashifashi na kupepea matawi ya miti huku wakiimba “Uhuru, Uhuru,” kama televisheni zilivyokuwa zikionesha.
Mpinzani mkuu wa Kenyatta, Waziri Mkuu Raila Odinga, aliibuka na kura 5,340,546 sawa na asilimia 43.28. Awali Mshauri wake wa karibu alisema hatakubali matokeo na atayapinga mahakamani kama Kenyatta atatangazwa mshindi.
“Hatakubali matokeo. Kama Uhuru Kenyatta atatangazwa Rais Mteule atakwenda mahakamani mara moja,” Salim Lone aliiambia Reuters, akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu.
Kambi ya Odinga ilisema wakati wa uhakiki, kwamba kazi ya kuhesabu kura ilivurugwa na kuomba isimamishwe.
Ili kupata ushindi wa moja kwa moja, mgombea alihitaji kupata asilimia 50 ya kura zote. Kenyatta ambaye ni Naibu Waziri Mkuu, alipata kiwango hicho lakini kwa tofauti ya kura 4,100 za zaidi ya kura milioni 12.3 zilizopigwa.
Ushindi wa raundi ya kwanza, ambao unapaswa kuthibitishwa rasmi na IEBC, inamaanisha kwamba Wakenya ambao walisubiri kwa siku tano kupata matokeo, sasa hawatakuwa na raundi ya pili ambayo ingesababisha wasiwasi wa muda mrefu. Mshindi pia anahitaji kupata angalau asilimia 25 ya kura katika majimbo 24 kati ya 47 yaliyopo.
Odinga pia alipoteza katika uchaguzi uliobishaniwa mwaka 2007 na kusababisha majuma kadhaa ya mapigano na mauaji ya kikabila. Kambi yake ilishasisitiza, kuwa kama kutatokea kutokubaliana na matokeo, njia watakayotumia ni inayozingatia utawala wa sheria, kwani Wakenya kwa jumla wana imani kubwa na Mahakama hivi sasa kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.
Waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo walisema wazi kwamba upigaji kura na kuhesabu kulifanyika kwa uwazi na Tume ya Uchaguzi ambayo iliahidi uchaguzi mzuri.
Matokeo mengine ya wagombea urais kwa mujibu wa Hassan ni James ole Kiyiapi (40,998); Martha Karua (43,881); Mohamed Dida (52,848); Musalia Mudavadi (483,981); Paul Muite (12,580) na Peter Kenneth (72,786).
Hassan aliwapongeza Kenneth na Mudavadi kwa kukubali kushindwa mapema na aliwataka walioshindwa wengine kuiga mfano huo ambao ni wa kiungwana.
Alipongeza pia Wakenya kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura akisema kati ya waliojiandikisha 14,315,533 ni wapiga kura 12,330,038 sawa na asilimia 86 walijitokeza kupiga kura.
Matokeo haya yataibua sintofahamu kwa wafadhili wakuu wa Kenya kutoka mataifa ya Magharibi, kutokana na Kenyatta kutarajiwa kwenda The Hague kusikiliza mashitaka dhidi yake ya kupanga machafuko ya kikabila miaka mitano iliyopita.
Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yalionya kabla ya uchaguzi, kwamba ushirikiano wa kidiplomasia unaweza kuwa mgumu kutokana na ushindi wa Kenyatta, ambaye mgombea mwenza wake William Ruto naye anakabiliwa na kesi hiyo.
Namna wafadhili wa Magharibi watakavyoshirikiana na Kenya chini ya Kenyatta na kiwango ambacho watakuwa tayari kuisaidia Serikali yake vitategemea zaidi jinsi Kenyatta na Ruto watakavyotoa ushirikiano kwa Mahakama hiyo.
“Haitaumiza kichwa kama atashirikiana na ICC,” alisema mmoja wa mwanadiplomasia wa Magharibi. “Tunaheshimu uamuzi wa wapigakura wengi wa Kenya.”
Kenyatta na Ruto walishakanusha mashitaka hayo na kusema watashirikiana ili kusafisha majina yao, ingawa Kenyatta alilazimika kujibu mapigo ya Odinga wakati wa kampeni ambapo alidai kuwa akishinda atalazimika kuendesha Serikali kwa njia ya kompyuta kutoka The Hague.
Lakini Wakenya waliendelea kuwa na matumaini kwamba uchaguzi huu utarejesha heshima ya taifa hilo kama moja ya nchi zenye demokrasia komavu katika Afrika hasa baada ya machafuko yaliyopita.
Jijini Kisumu, ambako ndiko ngome kuu ya kikabila ya Odinga na kitovu cha machafuko ya miaka mitano iliyopita, jana hali ilikuwa tulivu na kulionekana dhahiri kutokuwapo hamu ya ghasia, hata kama kuna baadhi waliamini kwamba uchaguzi ulivurugwa.
Hata hivyo, Odinga alitangaza jana kupinga matokeo hayo mahakamani. Alisema kulikuwa na matatizo katika uhakiki wa matokeo na kuwataka wafuasi wake kutulia wakati akitafuta faraja mahakamani.
“Kiwango cha mfumo mzima kushindwa kinasababisha ugumu wa kuamini kama matokeo hayo ni halali, na kama Uhuru atatangazwa Rais, Raila atakwenda mahakamani,” alisema mapema Mshauri wake Salim Lone.
Katibu Mkuu wa ODM, Anyang Nyong’o aliuambia mtandao wa Afrika Kusini wa Mail and Guardian Online, kwamba chama chake kitapinga mahakamani “kwa sababu mchakato umekuwa batili na kuna ushahidi”.
Kalonzo Musyoka, ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Odinga alisema IEBC inapaswa kubeba lawama kwa kuvuruga kazi ya kuhesabu kura.
Baada ya kutangaza matokeo ya urais, Mahakama Kuu ina siku 14 za kisheria za kutoa uamuzi juu ya pingamizi lolote dhidi ya matokeo.