WALIMU WAWEKA REHANI KADI ZAO ZA ATM KWA MIKOPO...

Mashine ya ATM.
Walimu zaidi ya 300 wilayani hapa wameweka rehani kadi za mashine za kutolea fedha benki(ATM) baada ya kukopa kwa watu binafsi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Dk Michael Kadege alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa kawaida wa mwaka wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos) cha walimu wilayani hapa kinachojumuisha pia wanachama kutoka wilaya ya Momba.
Alisema ni jambo la kusitikisha kwa walimu wanaoaminiwa na jamii kuwa werevu kujiingiza katika mikopo ya namna hiyo inayowalazimu kutoa pia namba zao za siri na kuruhusu wakopeshaji kwenda kujichukulia fedha benki mara mishahara inapotoka.
“Walimu wametoa kadi wakakabidhi na namba zao za siri hivyo mkopeshaji anaamua mwenyewe akatoe shilingi ngapi kwenye akaunti husika. Sijui walimu hawa wakitapeliwa na mkopeshaji wa namna hii watamfikisha katika chombo gani cha sheria kwa kuwa hakuna mkataba wowote waliowekeana,” alihoji Dk Kadege.
Alisema matokeo ya mikopo ya aina hiyo imekuwa ni walimu kushindwa kutimiza wajibu wao wa kufundisha badala yake wanautumia muda wa vipindi kufanya kazi mbadala, ikiwemo kuendesha bodaboda.
 Alisema hali hiyo inatokana na walimu kuchukua mikopo zaidi ya mishahara yao, kwani kupitia mpango huo wa kukopeshana kienyeji, haupo utaratibu wa ukomo wa mkopo kama ilivyo kwa mikopo inayotolewa kwa taratibu stahili.
Mkuu huyo wa wilaya aliusihi uongozi wa Saccos ya walimu kuhimiza walimu kujiunga na chama hicho waweze kukopa kwa taratibu zinazotakiwa na kuepuka mikopo ya kitapeli ambayo haiwezi kuwaletea manufaa kutokana na riba kubwa wanayotozwa.
Mmoja wa maofisa wa Benki ya CRDB mkoani Mbeya, Alpha Manota aliwasihi wateja wa benki kuacha tabia ya kuamini kila mtu katika jamii inayowazunguka kwa kutoa kadi ya ATM na namba ya siri.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item