MTALII ARUKA GHOROFANI AKIKIMBIA KUBAKWA HOTELINI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/mtalii-aruka-ghorofani-akikimbia.html
Taj Mahal. |
Mtalii wa Uingereza nchini India amelazwa hospitalini baada ya kuruka nje ya dirisha katika jaribio la kukimbia kubakwa, imefahamika.
Mwanamke huyo mwenye miaka 25 alikuwa anakaa katika hoteli katikati ya Agra, mji ilipo Taj Mahal, ndipo mtu mmpja alipovamia chumbani mwake na na kujaribu kumbaka.
Kisha mwanamke huyo akaruka kutoka dirisha la ghorofa ya kwanza na kupelekwa hospitali moja ya karibu kutokana na kupata majeraha kichwani na kuvunjika miguu yote miwili.
Mtuhumiwa huyo wa ubakaji, ambaye pia alikamatwa, anaaminika kuwa ni mmiliki wa hoteli hiyo ambako mtalii huyo alikuwa akiishi.
Msemaji wa Mamo ya Nje wa Uingereza alisema kwamba maofisa walikuwa 'wakichunguza haraka' taarifa hizo.
Habari zimekuja siku chache tu baada ya mtalii wa Uswisi kubakwa na genge la Wahindi huku mumewe akifungwa kwa kamba na kulazimishwa kutazama.
Shambulio hilo lilifanyika wakati watalii hao wakiendesha baiskeli wakiwa likizoni katika kijiji kisichofikika kwa urahisi cha Madhya Pradesh, lakini tukio karibuni linatia hofu zaidi kutokana na ukweli kwamba limetokea kwenye mji maarufu wa utalii unaotembelewa na mamilioni ya watu kutoka nchi za Magharibi kila mwaka kama sehemu ya vivutio vya 'Golden Triangle' kaskazini mwa India.
Suala la unyanyasaji wa kijinsia nchini India limechukua sura ya kipekee Desemba, baada ya mwanafunzi mwenye miaka 23 kubakwa kwenye basi na kusababishiwa majeraha makubwa na kisha baadaye kufariki dunia.
Shambulio hilo lilisababisha harakati za maandamano kitaifa kwa wanawake na wanaume kuvamia mitaa kudai adhabu kali kwa washambuliaji wa waathirika na ulinzi mkubwa dhidi ya matukio ya siku zijazo.
Serikali ya India limeweka sheria mpya ambayo itaongeza adhabu ya chini ya ubakaji hadi kifungo cha miaka 20 jela na kutoa adhabu ya kifo kwa matukio ambayo yatasababisha muathirika kufariki dunia.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza jana imeboresha ushauri wake wa safari kwa wanawake waliopanga kutembelea India, hususani kabla ya taarifa za hivi karibuni za jaribio la ubakaji.
"Wanawake wanatakiwa kuchukua tahadhari wanaposafiri kwenda nchini India." ulisema ushauri huo.
"Wanawake wa Uingereza wamekuwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia katika miji ya Goa, Delhi, Bangalore na Rajasthan."