AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUMNAJISI KUKU JIKE MUSOMA...

Kijana aliyejulikana kwa jina la Yusuph Bakari (28), Mkazi wa Kigera Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kunajisi kuku jike.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma alisema tukio hilo ni la Aprili 24 saa 3 asubuhi mwaka huu.
Mwakyoma alisema kuku huyo ni mali ya Nyamera Kitambara (26), ambaye ni mmiliki wa nyumba anayopanga mtuhumiwa.
Baada ya tukio hilo, mwenye nyumba alipiga yowe na wananchi walikwenda kumsaidia kumkamata kijana huyo na kumfikisha kituo cha Polisi. Kuku huyo alipelekwa kwa Ofisa Mifugo kwa ajili ya uchunguzi.
Wakati huo huo, mtoto mwenye umri wa miaka minane, Rhobi Marwa ameunguzwa mdomoni kwa moto wa kibatari na wifi yake,  akimtuhumu kunywa uji wa mwanawe.
Anayedaiwa kutenda kosa hilo ni Elizabeth Bureko (26), mkazi wa Nyamatare, Manispaa ya Musoma.
Anatuhumiwa kutenda kosa hilo juzi na amelazwa Hospitali  ya Mkoa wa Mara baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira, kutokana na kumwunguza mtoto huyo.
Mwakyoma alisema chanzo cha mwanamke huyo kufanya hivyo ni baada ya kumkuta wifi yake huyo akimpatia uji
mtoto wake, mwenye umri wa miezi miwili huku akilia.
Inadaiwa alimshutumu kuwa uji huo alikuwa anaunywa badala ya kumpa mtoto.
"Wananchi  walikerwa baada ya kuona kitendo hicho hivyo walianza kumpiga mama huyo na sasa amelazwa hospitalini kwa matibabu na akishapona sheria itachukua mkondo wake," alisema Mwakyoma.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item