AZUNGUKA MIGAHAWA 6,300 YA KICHINA, BADO HAWEZI KUTUMIA FIMBO ZA KULIA CHAKULA...

Mpenzi wa chakula cha Kichina amekula kwenye migahawa 6,300 tofauti na kusafiri kote Marekani akitimiza tamaa yake ya mapishi ya pande za Asia.

Lakini licha ya kula chakula cha Kichina kwa maisha yake yote, David Chan bado hawezi kutumia fimbo za kulia chakula.
Uchunguzi wa Chan ulianza kwa bidii baada kumaliza chuo pale alipojaribu kula katika kila mgahawa wa Kichina ulioko nyumbani kwake mjini Los Angeles.
Mapenzi yake kwa mapishi hayo mpaka sasa yamemfanya atembee kwenye majimbo 50.
Mhasibu huyo mwenye miaka 64 ameshachunguza kila mlo katika orodha na kwa zaidi ya miaka 58 iliyopita, Chan ameshajaribu mgahawa mpya wa Kichina kwa wastani wa kila baada ya siku tatu.
Ujasiri wake wa ajabu pengine ni wa kusifika zaidi kutokana na Chan kuwa akichukia zaidi vyakula vya Kichina wakati alipokuwa mtoto.
Mtu huyo wa kizazi cha tatu cha Waasia-Wamarekani alipendelea zaidi spageti au mkate wa nyama hadi alipogundua furaha za chakula cha Kichina wakati alipokuwa chuoni.
Umahiri kama huo wa Chana kwa chakula cha Kichina ambao migahawa inashutumu mara kashaa kumtaka kutoa maelezo kuhusu sehemu nzuri za kujaribu na pia ameandika kuhusu mapishi ya nchi hiyo na historia.
Alisema kwamba aligundua chakula cya Kichina kama njia ya kujiunganisha na utamaduni wake.
Wakati alipopata ajira yake ya kwanza, Chan alijiunga na kundi la wenzake kutoka Hong Kong na walijipanga kutoka kwenda kujaribu kila mgahawa watakaouona.
Chan alieleza: "Kila mara nimekuwa mkusanyaji. Nilikusanya stempu na santuri."
Hata hivyo mapenzi yake ya chakula cha Kichina hayakuanzia kutoka utotoni.
Anasema alikuwa amelelewa kama Mmarekani na wazazi wake ambao walitaka 'kumlinda' kutoka ubaguzi.
Wakati alipokuwa kijana migahawa pekee ya Kichina ilikuwa katika mji wa Chinatown na katika mwaka 1950 alikuwa ni mmoja kati ya watu 8,067 wa China waliokuwa wakiishi mjini Los Angeles.
Chan alieleza: "Isipokuwa tu unaishi mjini San Francisco, ulikuwa mgeni."
Uhamiaji China ulienea zaidi pale alipokuwa akisoma katika UCLA baada ya serikali kulegeza sheria ambazo zilikuwa zikiruhusu watu 105 kila mwaka kuhama kutoka nchini China kwenda Marekani.
Ilikuwa wakati wa miaka yake chuoni ndipo Chan alianza kujiunga na tamaduni za China na kuanza kozi iliyoitwa Mapishi katika Marekani.
Chan alisema moja ya sehemu zake za kuvutia za anavyopendelea ni kuona jinsi mapishi hayo yalivyoendelea kwa zaidi ya miongo.
Anasema amegundua michanganyiko ya Kimarekani-Kichina - kama sandwichi za Chow Mein zinazopatikana katika New England -  zinazovutia na kuburudisha kama utamaduni wa chakula cha Kichina.
Huku kukiwa na mgahawa mmoja tu ambao hurejea hapo, ABC Seafood, Chan alisema mgahawa huo namba moja wa sasa wa Kichina ni Koi Palace huko Daly City, California, ambako wamebobea katika kufifiliza wakati wa chakula cha mchana na mtindo wa Hong Kong wa chakula cha baharini wakati wa chakula cha usiku.
Mtoto wa kiume wa Chan, Eric anaamini tamaa ya baba yake imeanzia kutoka pale alipokuwa mkusanyaji wa asili.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item