BIBI MUUZA 'UNGA' ANAYESUBIRIA ADHABU YA KIFO HUKO BALI ATAMANI KUFA KWA RISASI....
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/bibi-muuza-anayesubiria-adhabu-ya-kifo.html
Bibi Lindsay Sandiford akifuma masweta ndani ya selo yake anakosubiria adhabu ya kifo huko Bali. |
Bibi wa Uingereza anayekabiliwa na hukumu ya kifo huko Bali amefanya mahojiano yake ya kwanza wakati akisubiria kifo - kwa ujasiri akiweka wazi yuko tayari kufa kwa kupigwa risasi.
Akizungumza kutoka kwenye selo yake ndani ya gereza mashuhuri la Kerobokan, Lindsay Sandiford alieleza: "Pengine ningependa hukumu ya kifo kuliko kifungo cha maisha. Sitaki kuzeeka na kuchakaa humu ndani ... angalau risasi ni haraka."
Ombi hilo lisilo la kawaida la bibi huyo mwenye miaka 56 limekuja baada ya rufaa yake dhidi ya hukumu yake kutupiliwa mbali Jumatatu, uamuzi ambao umeshutumia kama 'kioja na dhalimu'.
Shujaa wa dawa za kulevya Sandiford alikamatwa Mei mwaka jana baada ya kuingia Bali akitokea Bangkok akiwa amebeba cocaine zenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 1.6.
Katika mahojiano hayo - yaliyofanywa kupitia watu wa kati kwenye gereza hilo - alisema: "Sasa nimepata ugonjwa wa baridi yabisi. Nitakuwa nafananaje katika kipindi cha miaka kumi pale nitakapokuwa siwezi kutembea?
"wakati mwingine nafikiri, "Wacha wafanye watakavyo." Nilikuwa na furaha sana katika maisha yangu. Nilikwenda sehemu nyingi sana, kufanya vitu vingi mno na nimeshakutana na watu wengi wa kuvutia.
Sija majuto, ningeweza kufa kwa saratani au kingine cha kutisha na kurefushwa."
Baada ya kukamatwa kwake Sandiford alishirikiana na polisi katika oparesheni kali iliyopelekea kukamatwa kwa wanaodaiwa viongozi wa njama hizo.
Lakini wakati akihukumiwa kifo Januari, Waingereza wengine watatu - Julian Ponder, mwenye miaka 43, Paul Beale, miaka 40, na mshirika wa Ponder Rachel Dougall, miaka 38 - ambao walisemekana kuratibu shehena hiyo, walihukumiwa kifungo cha hadi miaka sita jela.
Mashitaka ya kusafirisha dhidi ya Ponder na Beale yalifutwa na walihukumiwa kifungo cha miaka sita na minne kwa kufuatana kwa kupatikana na dawa za kulevya, wakati Dougall anatarajia kuachiwa huru mwezi ujao baada ya kifungo cha mwaka mmoja kwa kushinda kutoa taarifa kuhusu uhalifu huo.
Pingamizi la Sandiford katika Mahamaka Kuu ya Bali dhidi ya hukumu yake lilitupwa licha ya ombi la kimaandishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza na Mkurugenzi wa zamani wa Mashitaka Lord MacDonald, ambaye alifafanua hitilafu katika hukumu kama 'isiyoweza kueleweka'.
Katika kioja cha vuta nikuvute, siku kadhaa tu baada ya hukumu, jaji wa kesi halisi alikutwa amekufa kutokana na kinachohisiwa ugonjwa wa moyo. Amser Simanjuntak, miaka 55, ilisemekana kuwa alianguka nyumbani kwake wakati akijiandaa kwenda kazini siku ya Ijumaa.
Sandiford, ambaye asili yake ni kutoka Redcar, Teesside, anapitisha muda wake akisubiria kifo - ambako jotoridi linafikia nyuzi 95F - akifuma masweta kwa ajili ya marafiki na familia yake kwao. Na licha ya kuiponda Mahakama Kuu kwa kutupa pingamizi lake, anasema hataki kuonewa huruma yoyote.