CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/cheka-taratibu_20.html
Jioni moja jamaa mmoja alikwenda kumtembelea rafiki yake. Wakati akiwa huko, mara mvua kubwa ikaanza kunyesha ndipo mwenyeji wake akasema: "Usijali rafiki yangu, utalala hapa sebuleni sababu mvua ni kubwa mno!" Jamaa akakubali. Mwenyeji wake akamuaga na kuingia chumbani kwake kulala. Usiku wa manane mwenyeji akaamka na kwenda sebuleni kumpelekea shuka mgeni wake na kukuta ameloa chapachapa. Mwenyeji akahoji kulikoni ndipo jamaa akajibu: "Nilikwenda nyumbani kuchukua shuka na mswaki!: Balaa...