WAFANYAKAZI 'WASALI' WAGONJWA WA AKILI MIREMBE WASIUAWE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/wafanyakazi-wagonjwa-wa-akili-mirembe.html
Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya wagonjwa wa akili ya Mirembe, mkoani Dodoma ambao shughuli kubwa ni kuwahudumia wagonjwa wa akili maisha yako hatarini kutokana na ukosefu wa dawa za wagonjwa hao.
Mfamasia Mfawidhi wa Hospitali ya Mirembe, Stella Mwaisaka aliwaambia wadau waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuwa hospitali hiyo kwa kipindi kirefu imekuwa na ukosefu wa dawa jambo ambalo linatishia maisha ya wafanyakazi.
Mwaisaka akichangia mada kwenye semina hiyo alisema kwa miaka miwili sasa tatizo la dawa za vichaa limekuwa sugu katika hospitali hiyo hali inayowafanya wagonjwa wa akili kuwa katika hali mbaya.
“Tatizo hili la dawa sasa ni kubwa wafanyakazi wa pale tutakufa,” alisema Mwaisaka na kueleza kuwa wanapoagiza dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa wanaeleza kuwa dawa hizo hazipo. Alisema wamefanya maombi maalumu ya dawa hizo, lakini yapata miaka miwili hawajaletewa dawa hizo.
Alisema kuwahudumia vichaa ni kazi ngumu na wafanyakazi wanajituma na juzi wamekwenda kanda ya MSD ya Dodoma wamepata dawa kidogo jambo ambalo alisema pia kuwa dawa hizo hazitoshelezi mahitaji ya wagonjwa wa hospitali hiyo.
“Noamba suala hili liangaliwe kuepusha wafanyakazi wasiuawe na vichaa,” alisema Mwaisaka na kueleza kuwa hata vitendea kazi katika hospitali hiyo ni vidogo na akatoa mfano wa dawa aina ya Antiseptics ambayo inatumika kusafishia mawodi nayo haipatikani.
Alitaja dawa ambazo ni zinatakiwa na hospitali hiyo kuwa ni Haloperidol, Blanzepine 10mg, phenobarbitone 100mg na Risperidone 1g. dawa hizo zinatumika kwa ajili ya kuwapatia wagonjwa wa akili ili waweze kuwa katika hali ya kawaida.
Alisema kutopatikana kwa dawa hiyo kumefanya wodi za Mirembe kuwa na harufu mbaya kwa sababu wagonjwa wa akili wanajisaidia ovyo na kufanya hali katika wodi za wagonjwa kuwa mbaya zaidi.
“Harufu ni mbaya mawodini isije ikafanya watu wakagoma kuingia mawodini na hatari nyingine wanaoingia kwenye mawodi yale kuna hatari ya kupeleka maambukizi kwenye familia zao,” alisema. Hospitali ya Mirembe ina wagonjwa wapatao 650.
Dawa ya antiseptics inatumika kufanyia usafi mawodini na inapunguza kukata harufu pamoja na kuua bakteria hatari wa magonjwa ya kuambukiza. Ukosefu wa dawa hiyo na vitendea kazi vingine kama glovu zinahatarisha maisha ya wafanyakaziwa hospitali ya Mirembe.
Akijibu hoja hiyo, Ofisa Mwandamizi wa MSD, Celestine Haule alisema ukosefu wa dawa za vichaa linatokana na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuzuia baadhi ya dawa zilikuwa zinaletwa na MSD kutoka nje ya nchi kwa madai kuwa hazijatimiza viwango.
Alisema ili dawa iletwe nchini ni lazima isajiliwe na TFDA, kwani ndio mamlaka iliyopewa jukumu hilo na akaeleza kuwa dawa zilizokuwa zinapelekwa Mirembe zimezuiwa na Mamlaka hiyo kwa kuwa hazijasajiliwa.
“Kwenye msafara wa ng’ombe anayetakiwa kwenda kasi ni yule aliyeko mbele, lakini anayechapwa ni huyu wa nyuma, hili suala la dawa za magonjwa ya akili ni suala la supply chain (mlolongo),” alisema Haule.
Haule aliongeza kuwa ni utaratibu wa nchi ambao imejiwekea kuwa dawa ambazo hazijasajiliwa na TFDA zisiingizwe nchini kwa hiyo, hiyo ndio faida ya mfumo huu,” alisema Haule.
Kuhusu malalamiko kuwa hospitali hiyo imetoa maombi maalumu ya dawa, lakini hadi sasa hawajaletewa hizo dawa, Haule alisema wamekuwa wanachelewa kununua dawa hizo kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano kati ya waagizaji na MSD.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifani alisema kwa sasa dawa za wagonjwa wa akili zipo MSD na akasisitiza kuwa ukosefu wa dawa hizo katika hospitali ya Mirembe unatokana na TFDA kupiga marufuku uingizaji wa dawa za msambazaji wa awali kwa maelezo kuwa hazikuwa na ubora.