MHADHIRI WA MAREKANI ABAKWA NA WANAUME TISA PAPUA NEW GUINEA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/mhadhiri-wa-marekani-abakwa-na-wanaume.html
KUSHOTO: Mhadhiri huyo baada ya kukatwa nywele na kubakwa. KULIA: Eneo la msitu ambako ubakaji huo ulifanyika. |
Mhadhiri mmoja wa Marekani amebakwa na kundi la askari tisa wenye silaha nchini Papua New Guinea ambao walikatakata nywele zake za rangi ya shaba na kumwacha mumewe akiwa amefungwa kwenye mti bila nguo.
Mwanamke huyo mwenye miaka 32, ambaye alikuwa akifanya utafiti kuhusu ndege wa ajabu kwenye msito uliojitenga katika Kisiwa cha Karkar, alikuwa akitembea kando ya kichaka na mumewe na mlinzi Ijumaa ndipo walipovamiwa na kundi hilo lenye silaha za visu na bunduki.
Mume wake na mlinzi walivuliwa nguo na kuzingirwa na wanaume hao, ambao baadaye walitumia kisu cha msituni kukata nywele za mwanamke huyo kabla ya kumbaka katika tukio la kutisha lilichukua dakika 20.
Mwanamke huyo alichagua kuzungumzia hadharani shambulio hilo la kutisha - lililoshutumiwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Peter O'Neil kama 'kitendo cha kinyama' - akimulika shambulio ambalo amekumbana nalo mwanamke huyo nchini Papua New Guinea.
Tukio hilo la kubakwa na kundi limekuja chini ya kipindi cha wiki moja baada ya mtu mmoja wa Australia anayeishi kwenye milima ya kati ya Papua New Guinea kufa kwa kupigwa risasi na rafiki yake wa kike kutoka Filipines kubakwa na kundi la wanaume waliovunja na kuingia nyumbani kwake.
Mwanamke huyo wa Marekani, ambaye hakutaka kujitambulisha, alizungumza kwenye vyombo vya habari mjini Port Moresby huku yeye na mumewe wakisubiria ndege kuondoka nchini humo.
"Nilikuwa nikitembea kwenye njia kando ya msitu na mume wangu na mlinzi wetu ndipo tukazingirwa na wanaume tisa wenye silaha bunduki na visu," alisema.
Akielezea tukio hilo ambalo limeshitua kote nchini humo, mwanamke huyo alisema wanaume hao kwanza walimwamuru mume wake na mlinzi kuvua nguo zote na kubaki uchi kabla ya kufungwa kwenye miti.
Nguo zake zilichanwa, mikono yake ilifungwa na nywele zake za rangi ya shaba zilikatwa katwa kwa kutumia visu vya msituni. Kisha baadaye akabakwa mmoja baada ya mwingine na kundi hilo kwa dakika 20 za mateso makali.
Mateso yake yalikoma tu pale kitu fulani kilipolishitua kundi hilo na wakatimua mbio kusikojulikana.
Mlinzi wa wapenzi hao wa Marekani alifanikiwa kujinasua na kuwafungulia wanandoa hao, kabla ya wote kutimua mbio wakiwa uchi katika njia za kando ya msitu mnene kwa masaa kadhaa, wakidhamiria kwenda umbali mrefu kadri inavyowezekana mbali na eneo la tukio la shambulio hilo kwa tahadhari endapo kundi hilo lingerejea pale.
Hatimaye walifika kwenye kijiji kimoja kilichojitenga ambako walipatiwa nguo na kutokea hapo waliweza kutoa taarifa hizo.
Baadaye walianza safari kurejea Madang, pwani ya kaskazini mwa bara, kabla kusafiri kwa ndege kwenda mji mkuu wa Port Moresby.
Mpigapicha mmoja wa eneo hilo anayefanyia kazi shirika la AFP aliwasaidia wanandoa hao kuandika maelezo polisi na kuandaa usafiri wa ndege kuondoka nchini humo.
"Simulizi hii haikutoka hadharani sababu tu mimi ni mzungu," alisema mwanamke huyo, ambaye ilikuwa safari yake ya tano kutembelea nchi hiyo tangu alipofanya safari yake ya kwanza mwaka 2010.
Ilikuwa akae kwa miezi hadi minne akifanya utafiti wake kuhusu ndege wa ajabu na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye msitu huo.
"Simulizi yangu imekuja hadharani kwa matumaini kwamba itawawezesha wanawake wa Papua New Guinea kusimama kidete na kukataa udhalilishaji dhidi ya wanawake katika nchi hii," alisema mwanamke huyo, ambaye hajutaka kujitambulisha.
"Nina imani simulizi yangu italeta mabadiliko."
Lakini polisi wa ngazi ya juu wanakiri wamesikia wito kama huo kabla kutoka kwa wanawake wa vijijini kote nchini Papua New Guinea.
Wake wanakabiliwa na unyanyasaji mkubwa katika baadhi ya kesi kutoka kwa waume zao kuhusu mambo ya kifamilia, na adhabu kali zinatolewa kwa wanawake wanaotuhumiwa kwa uchawi, ambavyo vinafanyika kwenye sehemu zilizojitenga za nchi hiyo.
Februari mama mwenye miaka 20 aliyetuhumiwa kwa uchawi alikokotwa kutoka kijini kwake, na kutupwa kwenye dampo la takataka, akavuliwa nguo na kuchomwa moto akiwa hai karibu na Mlima Hagen, katikati ya nchi hiyo.
Na mapema mwezi huu mwanamke mzee alikatwa kichwa kwa kutumia kisu cha msituni baada ya kuwa ametuhumiwa kwa uchawi.
Habari ya kutisha ya mwanamke huyo wa Marekani imeripotiwa kwa Ubalozi wa Marekani mjini Port Moresby, lakini ofisa wa zamu leo hakutoa maoni yoyote.
Msemaji wa polisi mjini Port Moresby alisema taarifa hiyo imepokelewa lakini hakuna yeyote aliyekamatwa mpaka sasa.