UADILIFU WA KIFEDHA SERIKALINI WAIMARIKA...

Janeth Mbene.
Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, amesema   uadilifu na uaminifu katika usimamizi wa fedha kwenye wizara na idara, umekuwa mkubwa kwa sasa na hiyo imesaidia mapato kuongezeka.

Mbene alisema hayo jana akifungua mafunzo ya awamu ya nne ya usimamizi wa fedha na uboreshaji, yaliyofanyika jijini hapa.
Alisema kutokana na kuongezeka kwa uadilifu,  hata Bajeti ya Serikali imeongezeka na kufikia Sh trilioni 17 kwa mwaka, tofauti na miaka mitano iliyopita.
Waziri alisema mageuzi yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kusimamia matumizi ya fedha za Serikali, na kutokana na hali hiyo, aliwaasa watendaji kutumia mafunzo hayo kujiendeleza na kuendelea na moyo huo wa uaminifu.
Msimamizi Mkuu wa Wizara ya Fedha, Fatima Kiongosya, alisema usimamizi mzuri na uadilifu katika sekta ya fedha, umefanya mahesabu ya Serikali yatolewe kwa wakati.
Kiongosya alisema hali hiyo sasa inampa nafuu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika kufanya kazi zake kwa uhakika.
Alisema changamoto zinazowakabili, ni ukusanyaji usiokidhi haja wa mapato katika halmashauri nchini, na   ndiyo maana wakaamua kuandaa mafunzo hayo, ili watendaji wafanye kazi yao kwa uhakika zaidi na pato la Taifa liongezeke.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item