WAKAMATWA KWA KUPANGA NJAMA ZA KUWAPIKA NA KULA WANAWAKE, WATOTO...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/wakamatwa-kwa-kupanga-njama-za-kuwapika.html
Robert 'Chris' Asch. |
Mkutubi wa zamani wa shule moja ya sekondari ya juu na mkuu wa gereza wamekamatwa jana kwa kula njama ya kuwateka nyara, kupika na kisha kuwala wanawake na watoto.
Kukamatwa kwa watu hao wawili Jumatatu asubuhi kumekuja kufuatia uchunguzi dhidi ya 'askari mla-watu' Gilberto Vale ambaye alitiwa hatiani kwa mashitaka kama hayo mwezi uliopita.
Robert 'Chris' Asch, umri wa miaka 61, ni mkutubi wa zamani kutoka Shule ya Sekondari ya Juu ya New York's prestigious Stuyvesant ambaye alikamatwa na FBI nyumbani kwake huko Greenwich Village Jumatatu asubuhi.
Katika maelezo kwenye mtandao, Asch alishirikisha ndoto zake hizo za kutesa na kubaka mwanamke, na alitarajia kufanya hivyo kwa kushirikiana na kundi la wanaume wenye akili kama zake.
Anayedaiwa kuwa mshirika wake katika mpango huo Richard Meltz, mwenye umri wa miaka 65 ambaye alikuwa mkuu wa polisi katika hospitali ya wakongwe mjini Massachusetts, naye pia alikamatwa Jumapili huko Rockaway, New Jersey.
Imeripotiwa kwamba Asch na Meltz walishitakiwa kwa njama ya utekaji nyara.
FBI haikufafanua jinsi Asch na Meltz walivyounganishwa na Vale, lakini imeripotiwa kwamba ofisa wa siri alitumika katika kuchunguza njama zao hizo.
Imeripotiwa kwamba FBI walianza mawasiliano na Asch pale alipojibu tangazo la kwenye mtandao ambako mtu mmoja alituma kwamba alikuwa akitaka msaada wa kuwateka nyara, kubaka na kuwaua mke wake, shemeji yake na watoto wa shemeji yake.
Tangazo hilo lilitumwa Oktoba na Asch alikutana na mawakala wa siri wa FBI kujadili njama zinazofanana na hizo katika miezi ya karibuni.
Katika mikutano miwili kati ya hiyo, aliwasilisha vitu ambavyo aliripotiwa kudhani vitatumika ikiwamo kofia nyeusi ya kufunika uso, pingu, nyundo, playa na koleo.
Mawakala hao waliandaa kiasi kwamba Asch afanye upelelezi dhidi ya mwanamke mmoja - bila kufahamu kwamba pia alikuwa mmojawapo katika mpango huo wa siri.
Wakati wa moja ya majadiliano na mkutano mwingine pamoja na mawakala, Asch aliripotiwa akisema shabaha ya mwanamke huyo 'lazima afe'.
Asch ndiye aliyemleta Meltz katika mpango huo, akisema kwamba alitaka kusaidia katika utekaji nyara wa mwanamke huyo.
"Huu ni mpango wa hatari kubwa," Asch alisema kwenye mahojiano yaliyorekodiwa akiwa na Meltz.
Kujaribu kumnyakua mtu mtaani, kuvamia nyumba, nafikiri ni hatari kubwa.
"Namaanisha, kuna njia kutenganisha viungo na kuangamiza."
Taarifa chache kuhusu njama zao zimebainishwa, lakini baadhi ya walengwa wao wanasemekana kuwa ni watoto wadogo.
Hii si mara ya kwanza kwamba Asch, ambaye amejitangaza kuwa shoga, kukamatwa.
Mahusiano ya Asch na watoto hapo kabla yaliibua maswali pale alipokamatwa na kusimamishwa kazi Stuyvesant mwaka 2009.
Kufukuzwa kwake kulikuja baada ya kudaiwa kuwatomasa wanafunzi wanne wa kiume katika sekondari hiyo ya juu na kunong'oneza katika moja ya masikio yao. Mashitaka hayo yalitupwa.
Wakala wa FBI walionekana wakipekua nyumbani kwa Asch kwenye jengo la St Germain lililoko Mtaa wa Greenwich muda mfupi baada ya kukamatwa kwake majira ya Saa 5 asubuhi.
Jirani mmoja katika jengo lake alisema kwamba wakazi wengine wakiwamo waigizaji kadhaa, baadhi yao wamewahi kucheza filamu za mauaji katika majukumu yao.